FIFA yasitisha rasmi kuja Tanzania na imebariki maamuzi ya Kisheria ya Mahakama dhidi ya Malinzi

FIFA yasitisha rasmi kuja Tanzania na imebariki maamuzi ya Kisheria ya Mahakama dhidi ya Malinzi

si ajabu fifa waliambia rais wa sasa wa Tanzania huwa hajaribiwi wakija huenda na wao wakalala ndani wakaamua waishie hukohuko
 
si ajabu fifa waliambia rais wa sasa wa Tanzania huwa hajaribiwi wakija huenda na wao wakalala ndani wakaamua waishie hukohuko
Mbona kuna wezi walikuja wakatinga mpaka KWA sisonje afu wakaishia kuitwa awa ndo wanaumee[emoji33] [emoji33] [emoji33]
 
Nilisema kuwa ningerudi tena JF muda wa Saa 5 usiku na muda ule nilioleta huu uzi ulikuwa ni Saa 3 kamili na kuna mahala nilikuwa nawahi. Suala siyo kuleta taarifa rasmi bali nilisema nitarudi ili tuendelee ' kuyajenga ' juu ya hili. Na cha ' kuchekesha ' kale ' Kabinti ' Makamu wa Kamati ya Uchaguzi kamesikika kakisema kuwa ' Yeye ' hana hiyo taarifa wakati ' waliovujisha ' hii taarifa ambayo bado inafanywa ' Siri ' ni hao hao ' Wajumbe ' wa Kamati hiyo pamoja na mmoja wa Mawakili wake kati ya wale Watano wanaomtetea Malinzi.

Nadhani TAKUKURU / PCCB iwakamate na hawa ' Wajumbe ' wanne ( 4 ) wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF ambao wanampigia ' chapuo ' Rais Malinzi ili wawahoji vizuri ' Kinjagu ' kwani yawezekana kuna ' chenji chenji ' ya Pesa anazotuhumiwa nazo Malinzi na wao ' wamegawiwa '.

Tusipoangalia hawa ' Wajumbe ' wabishi wanne ( 4 ) wa Kamati ya Uchaguzi Mkuu wa TFF wanaweza ' wakatucheleweshea ' maendeleo ya mpira wetu Tanzania na sidhani kama wana nia njema na mpira wa Tanzania kwani wamekaa ' Kimahaba ' na ' Kimaslahi ' zaidi.
kwa kweli takukuru iwashughulikie hawa wajumbe watatu wa hii kamati ya uchaguzi, hususan yule mama, na Justina Wambura. watu wana mpigia chapuo kwa kutumia wingi wao badala ya kanuni na taratibu. ndio maana mpira wetu ulikuwa hauendelei zaidi ya uongozi mbovu
 
Kesi ya ubadhikifu wa fedha FIFA wasingeliweza kuingilia mahakama ya Tz. Niliwaeleza humu mapema kua wanabwabwaja haiwezekani. Sasa mme amini maneno yangu? Mda wa kupiga umeisha.
 
EFM nao wajibadilishe maeneo mengi Tanzania hawasikiki hata huku nilipo hawasikiki wacha Clouds Fm iendelee kuwakimbiza.
 
Kuna kitu bado najiuliza. Hivi ile barua ya Malinzi ya kuomba kufanyiwa usaili kupitia nyaraka alizowasilisha zilifuata taratibu za mtu aliye rumande? Kwa jinsi ninavyofahamu ni kwamba barua zote zinazoandikwa na mahabusu lazima ziidhinishwe na Bwana Jela.
 
Fifa ya blatter na CAF ya Issa hayatou ndio zilikuwa zinaziba mabaya yao yote kuzuia serikali zisiingilie michezo, hiyo yote ilikuwa njama ya kulinda ubadhirifu wao
Lakini si nae huyo Blatter alishughukikiwa na FBI kwa tuhuma za rushwa na mengineyo akiwa anaelekea kwenye uchaguzi? Au ni Blatter yupi unaemsema wewe? Mfumo wa FIFA haujabadilika na unazitambua taasisi za kuzuia na kupambana na rushwa ndio pekee zinazotambuliwa na FIFA kuwa na uwezo wa kuingilia chama cha soka cha nchi husika pale zinapoona mambo yameenda ndivyo sivyo.
 
Kesi ya ubadhikifu wa fedha FIFA wasingeliweza kuingilia mahakama ya Tz. Niliwaeleza humu mapema kua wanabwabwaja haiwezekani. Sasa mme amini maneno yangu? Mda wa kupiga umeisha.
Mkuu tuko pamoja
 
Back
Top Bottom