FIFA yasitisha rasmi kuja Tanzania na imebariki maamuzi ya Kisheria ya Mahakama dhidi ya Malinzi

si ajabu fifa waliambia rais wa sasa wa Tanzania huwa hajaribiwi wakija huenda na wao wakalala ndani wakaamua waishie hukohuko
 
si ajabu fifa waliambia rais wa sasa wa Tanzania huwa hajaribiwi wakija huenda na wao wakalala ndani wakaamua waishie hukohuko
Mbona kuna wezi walikuja wakatinga mpaka KWA sisonje afu wakaishia kuitwa awa ndo wanaumee[emoji33] [emoji33] [emoji33]
 
kwa kweli takukuru iwashughulikie hawa wajumbe watatu wa hii kamati ya uchaguzi, hususan yule mama, na Justina Wambura. watu wana mpigia chapuo kwa kutumia wingi wao badala ya kanuni na taratibu. ndio maana mpira wetu ulikuwa hauendelei zaidi ya uongozi mbovu
 
Kesi ya ubadhikifu wa fedha FIFA wasingeliweza kuingilia mahakama ya Tz. Niliwaeleza humu mapema kua wanabwabwaja haiwezekani. Sasa mme amini maneno yangu? Mda wa kupiga umeisha.
 
EFM nao wajibadilishe maeneo mengi Tanzania hawasikiki hata huku nilipo hawasikiki wacha Clouds Fm iendelee kuwakimbiza.
 
Kuna kitu bado najiuliza. Hivi ile barua ya Malinzi ya kuomba kufanyiwa usaili kupitia nyaraka alizowasilisha zilifuata taratibu za mtu aliye rumande? Kwa jinsi ninavyofahamu ni kwamba barua zote zinazoandikwa na mahabusu lazima ziidhinishwe na Bwana Jela.
 
Fifa ya blatter na CAF ya Issa hayatou ndio zilikuwa zinaziba mabaya yao yote kuzuia serikali zisiingilie michezo, hiyo yote ilikuwa njama ya kulinda ubadhirifu wao
Lakini si nae huyo Blatter alishughukikiwa na FBI kwa tuhuma za rushwa na mengineyo akiwa anaelekea kwenye uchaguzi? Au ni Blatter yupi unaemsema wewe? Mfumo wa FIFA haujabadilika na unazitambua taasisi za kuzuia na kupambana na rushwa ndio pekee zinazotambuliwa na FIFA kuwa na uwezo wa kuingilia chama cha soka cha nchi husika pale zinapoona mambo yameenda ndivyo sivyo.
 
Kesi ya ubadhikifu wa fedha FIFA wasingeliweza kuingilia mahakama ya Tz. Niliwaeleza humu mapema kua wanabwabwaja haiwezekani. Sasa mme amini maneno yangu? Mda wa kupiga umeisha.
Mkuu tuko pamoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…