FIFA yawafungia Simba Sports Club Kusajili Ndani mwaka mmoja Kwa Kosa La Kutomlipa Asante Kwasi

FIFA yawafungia Simba Sports Club Kusajili Ndani mwaka mmoja Kwa Kosa La Kutomlipa Asante Kwasi

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Wakuu Imekuaje Tena Kemcho akashindwa Kumlipa Asante Kwasi?[emoji849][emoji849]

FIFA imeifungia simba kusajili kwa kipindi kimoja kijacho cha usajili. Nyundo hiyo ya FIFA imekuja kufuatia kuikuta na hatia Simba kutokana na kushindwa kumalizana na beki wao wa zamani, Mghana A. Kwasi. adhabu hiyo kwa Simba itaanza kufanya kazi katika dirisha lijalo la usajili
1619187787056.png

Asante Kwasi (kushoto) alipokuwa Simba

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limeifungia klabu ya Simba kusajili katika kipindi kimoja cha dirisha hilo kufuatia kutiwa hatiani kwa kutomlipa stahiki zake aliyekuwa beki wao raia wa Ghana, Asante Kwasi.

Adhabu hiyo imekuja kufuatia FIFA kujiridhisha kuwa Simba haikufanikiwa kumalizana na beki huyo baada ya kuachana naye mara baada ya kumalizika kwa msimu wa 2018/19 na kutakiwa kumlipa mchezaji huyo kiasi cha Sh. 25 milioni.

Simba itaanza kutumikia adhabu hiyo kuanzia msimu ujao katika dirisha kubwa la usajili litakalofunguliwa mara baada ya Ligi kumalizika.

Kwasi alijiunga na Simba mwaka 2017 akitokea klabu ya Lipuli FC ya mkoani Iringa iliyokuwa inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

====

Tanzanian giants Simba SC have been sanctioned by FIFA after failing to settle Ghanaian defender Kwasi Asante.

The talented right-back left Simba SC for Hafia in 2019 as a free agent with the Tanzanian side still owing him salaries and all efforts to get his money has proven futile.

Sportsworldghana.com understands that Asante dragged Simba to FIFA nad after several warnings which all fell On deaf ears, they have been banned from signing any player in the coming transfer window until they pat the Ghanaian player.

Asante previously played for Mbabane Swallows, Manzini Wanderers and a host of other teams.
 
kitengo cha propaganda za Yanga huwa kinajua kucheza vizuri kuelekea mechi ya watani
Achana na Mpira Twende Kwenye Jukwaa La Basketball [emoji3][emoji3][emoji3]
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Wala hakuna kinachoharibika Simba wala haina mapungufu ya kikosi.
Kina Manula wasiuzwe tu, bado Simba inaweza kutoboa.
 
Ukiwaaambia mbumbumbu fc Yanga na Simba ziko vilevile hakuna kilicho badilika Wana bisha. Izo timu Zina bebwa na fedha za watu MO na GSM ao jamaa wakiondoka hakuna chochote kinacho fanyika. Hizo timu hazina msingi wowote wa kuji beba.
 
Ukiwaaambia mbumbumbu fc Yanga na Simba ziko vilevile hakuna kilicho badilika Wana bisha. Izo timu Zina bebwa na fedha za watu MO na GSM ao jamaa wakiondoka hakuna chochote kinacho fanyika. Hizo timu hazina msingi wowote wa kuji beba.
Huo ndiyo ukweli....wakiondoka tu hao ni full mabakuli, majungu, kushikana uchawi.
 
Izo ni tetesi na hakuna taarifa rasmi
 
Back
Top Bottom