FIFA yazindua uwanja wa Pele Nchini Rwanda. Je, kwa Tanzania kiwanja gani kipewe jina la Pele?

FIFA yazindua uwanja wa Pele Nchini Rwanda. Je, kwa Tanzania kiwanja gani kipewe jina la Pele?

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino amezindua KigaliPeleStadium, wenye uwezo wa kuchukua watu 22,000 kwa heshima ya aliyekuwa nguli wa soka kutoka Brazil Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pelé, aliyefariki Desemba, 2022.

Hadi sasa 'Viwanja vya Pele' duniani ni Estádio Rei Pelé - Brazil, Estadio Bello Horizonte Rey Pelé - Colombia, Estádio Nacional de Cabo Verde - Cape Verde, Estádio Pelé - FIFA Zürich' na Kigali Pelé Stadium - Rwanda.

Je, kwa Tanzania kiwanja gani kipewe Jina la Pele?
 
Mpaka sasa hivi bado tukumbushane swala la picha kwa habari kama hii?

3e4b42bb-af65-4fd4-bdc7-c3f8ecde4d63.jpg
 
Rwanda kuna viwanjwa vikali sana vya basket ball ( vidogo ) ,
Yani ukipiga picha ni kama mbele
 
Kagame ni mjanja kiuchumi, ananunua madini kwa bei poa hasa kwa wale waliolalia masikio na kwenda kuuza kwa bei ya juu.
 
Uwanja wa kuchukua watu 22,000 ni uwanja wa halmashauri ya wilaya tu huku bongo.
Duh acha masihara Azam embu nitajie viwanja vinavyoingiza watu 22000 Tanzania ukitoa taifa, tena vyenye facilities zote za kisasa
 
Sasa mzee yani nchi ijenge uwanja kwa gharama zao afu uitwe kwa jina la mtu wa nje tena ht hana uhusiano wowote na nchi yako unaona ni sawa.?
Hapa Tanzania Kuna barabara ngapi au mitaa mingapi Ina majina ya watu ambayo sio watanzania???
Kibaki road, moi avenue na utitiri mwingine wa majina!!!

Usilete excuse kua ni viongozi sijui wa nchi au, stadium ni ya mpira na Pele ndio icon wa mpira Duniani sioni tatizo lolote?
 
Back
Top Bottom