MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
MATOKEO: Bondia Anthony Joshua wa Uingereza amefanikiwa kuchukua mkanda wa WBO baada ya kumpiga kwa points bondia Joe Parker wa New Zealand
Majaji katika ngumi hizo walimpa Joshua ushindi wa 118 - 110, 118 - 110, 119 - 109
Joshua sasa anamiliki mikanda ya WBO, IBF, IBO,WBA na amebakiza WBC unaomilikiwa bondia Deontay Wilder wa Marekani.
======================
Hatimaye siku imewadia, mpambano usiotabirika kati ya Anthony Joshua na Joe Parker unatarajia kuvuta washabiki wa ngumi duniani.
Wote wakiwa hawajawahi kupoteza pambano lolote na wakiwa miongoni mwa mabondia bora wa zama hizi wanatarajia kuthibitishia dunia kuwa ni mabondia wasiopigika.
Joe Parker anatarajiwa kubadili kile kilichoshinda wengi akiwemo mkongwe Klitschko kwa kumlambisha sakafu Anthony Joshua.
Lakini Anthony Joshua ambaye kwasasa ndie star wa masumbwi duniani na mwenye washabiki kuliko bondia yeyote duniani anatarajiwa kushinda pambano hili kutokana na rekodi yake.
Anthony Joshua kama leo akishinda atakuwa amechukua mikanda minne kati ya mitano ya ubingwa wa dunia! Mkanda utaobakia wa WBC upo kwa Deontay Wilder.
Kama akichukua na huo atakuwa undisputed heavyweight champion of the world ikiwa ni mara ya kwanza kwa bondia kutoka UK baada ya Lennox Lewis miaka ya mwanzoni ya 2000.
What is your final predictions?