Fight Night: Anthony Joshua ampiga kwa points Joe Parker

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583


MATOKEO: Bondia Anthony Joshua wa Uingereza amefanikiwa kuchukua mkanda wa WBO baada ya kumpiga kwa points bondia Joe Parker wa New Zealand

Majaji katika ngumi hizo walimpa Joshua ushindi wa 118 - 110, 118 - 110, 119 - 109

Joshua sasa anamiliki mikanda ya WBO, IBF, IBO,WBA na amebakiza WBC unaomilikiwa bondia Deontay Wilder wa Marekani.

======================

Hatimaye siku imewadia, mpambano usiotabirika kati ya Anthony Joshua na Joe Parker unatarajia kuvuta washabiki wa ngumi duniani.

Wote wakiwa hawajawahi kupoteza pambano lolote na wakiwa miongoni mwa mabondia bora wa zama hizi wanatarajia kuthibitishia dunia kuwa ni mabondia wasiopigika.

Joe Parker anatarajiwa kubadili kile kilichoshinda wengi akiwemo mkongwe Klitschko kwa kumlambisha sakafu Anthony Joshua.

Lakini Anthony Joshua ambaye kwasasa ndie star wa masumbwi duniani na mwenye washabiki kuliko bondia yeyote duniani anatarajiwa kushinda pambano hili kutokana na rekodi yake.

Anthony Joshua kama leo akishinda atakuwa amechukua mikanda minne kati ya mitano ya ubingwa wa dunia! Mkanda utaobakia wa WBC upo kwa Deontay Wilder.

Kama akichukua na huo atakuwa undisputed heavyweight champion of the world ikiwa ni mara ya kwanza kwa bondia kutoka UK baada ya Lennox Lewis miaka ya mwanzoni ya 2000.


What is your final predictions?
 

Attachments

  • Screenshot_20180331-140509.jpg
    35.8 KB · Views: 92
  • FB_IMG_1522494386329.jpg
    51.9 KB · Views: 105
Mapema kabisaa tunachukua ushindi na mpira tunatia kwapani[emoji119][emoji16][emoji123]..team Joshua the best Boxer
 
Joshua atafia uwanjani leo.

Parker ni moto wa kuotea mbali
 
Ngj tusubirie...ni Ngumu kujua mshindi kwenye pambano Hilo

Ova
 
Mechi inaisha kwa t.k.o joshua anashinda kwa sabb zfuatazo,,,,power punches,stamina,combination of punches na sahv amepunguza uzito sana kwnye hili pambano compared na mapambano ya nyuma so tutegemee atakua na speed zaidi uck wa leo ukijumlisha na physical appearance anashindaa kwa kishindo zaidi ya huyo samoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…