Fight night: huku Canelo Alvarez kule Kamaru Usman

Naona Canello ana record na experience yakutosha, hapo nampa nafasi kubwa ya ushindi.
Lolote linaweza tokea kwenye ndondi.
Kwenye mchezo wa AJ na Oleksandr Usyk asilimia kubwa watu walimpa AJ kama atashinda kutokana na records na experience lakini matokeo yalikuwa tofauti
 
Mwaka 2019 Kamaru Usman ambaye ni mzaliwa wa Nigeria alifanikiwa kuwa mwafrika wa kwanza kutwaa mkanda wa UFC kwenye uzito wa Welterweight baada ya kumpiga Tyron Woodley aliyekuwa akishikilia mkanda huo, amefanikiwa kuulinda mkanda huo hadi sasa, amekuwa very impressive kiasi cha kuwekwa kwenye 'Goat discussion' wa UFC sambamba na majina makubwa kama Jon Jones, Khabib, na GSP. Je kesho ataendelea kuboresha legacy? Time will tell...
 
Mabingwa wa UFC kutoka Afrika;

1. Kamaru Usman--- Welterweight
2. Francis Ngannou---Heavyweight
3. Israel Adesanya---Middleweight
 
Kwenye boxing sina wasiwasi Canelo anashinda.

Shughuli ipo hapo UFC. Natamani sana Kamaru Usman "the Nigerian Nightmare" ashinde ila Colby yupo vizuri zaidi.

Pambano lao la kwanza Kamaru alinyamazisha ukumbi uliokuwa umejaa mashabiki wa Colby kwa KO Raundi ya mwisho.

Kinachomsaidia Kamaru Usman ni utulivu na uvumilivu akiwa ndani ya Cage.
Colby yupo vizuri ila tatizo ana dharau na majivuno sana dhidi ya wapinzani wake.

Tukutane baadae kwa updates na live streaming.
 
Lolote linaweza tokea kwenye ndondi.
Kwenye mchezo wa AJ na Oleksandr Usyk asilimia kubwa watu walimpa AJ kama atashinda kutokana na records na experience lakini matokeo yalikuwa tofauti
Boxing ina matokeo ya kushangaza sana, ndo maana huwa naogopa kutabiri
 
Mi nahisi hii ngoma inaisha mapema kuliko ile ya mwanzo, Kamaru amekuwa bora zaidi ya jana[emoji2][emoji2]
 
Mi nahisi hii ngoma inaisha mapema kuliko ile ya mwanzo, Kamaru amekuwa bora zaidi ya jana[emoji2][emoji2]
Sio rahisi hivyo mkuu.

Hata Colby atakuwa amefanyia kazi makosa yake ya mwanzo, hasa lile kosa la kumsogezea uso Kamaru.

Usijaribu kubet kwenye hili pambano maana lipo 50/50, atakayezubaa kidogo anamalizwa.
 
Sio rahisi hivyo mkuu.

Hata Colby atakuwa amefanyia kazi makosa yake ya mwanzo, hasa lile kosa la kumsogezea uso Kamaru.

Usijaribu kubet kwenye hili pambano maana lipo 50/50, atakayezubaa kidogo anamalizwa.
Hakuna betting ngumu kama za MMA maana yeyote anakalishwa inategemea umeotewa vipi, mtu pekee ambaye ukiweka mzigo ilikuwa uhakika alikuwa Khabib [emoji16][emoji16]
 
Haya ni maoni ya mdau mmoja kuhusu haya mapambano ya kesho, kesho sio battle ya wapiganaji tu bali pia ni battle ya two combat sports (BOXING vs MMA). Miaka ya hivi karibuni imekuwa ni miaka mizuri kwa Martial Arts (UFC) kwani wamefanikiwa kuandaa PPV events nyingi na kufanikiwa sana kiasi cha kuupiku mchezo mkubwa wa Boxing, wamefanikiwa kuutumia udhaifu wa wa uendeshaji wa Boxing kuweza kwenda juu. Ikumbukwe mwaka juzi wakati Canelo ambaye ndio biggest star kwenye boxing akipigana na Kovalev, siku hiyohiyo kulikuwa na pambano la Jorge Masvidal vs Diaz (UFC244), ikawalazimu upande wa Canelo wasogeze muda wa pambano ili kupisha UFC event kwisha kwakuwa kwa kiasi kikubwa mashabiki wanaofatilia MMA ndio wanaofatilia Boxing. Je na kesho itatokea hivyo? Maana UFC wana mtaji wa mapambano matatu makubwa hivyo kuwa tishio kwa pambano la Canelo na Plant
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…