Fight night: huku Canelo Alvarez kule Kamaru Usman

Fight night: huku Canelo Alvarez kule Kamaru Usman

UFC: Kamaru won by UD. Very close fight, respect kwa Colby
 
Canelo record yake iko vzuri zaidi. Ila kwann mabondia wengi mkao wao ni Orthodox!?
Kwasababu binadamu wengi mkono wa kulia ndio una nguvu zaidi
 
Jumamosi ijayo, T-MOBILE Arena Las Vegas kinanuka!!!

Legacy is earned, wameiita hivyo wenyewe
 
Canelo vs Bovol, pambano gumu sana
 
Canelo leo kawa nyanya, anachezea kichapo cha Bivol
 
Jumamosi kuamkia jumapili hii (tar 6-7) ni siku kubwa kwa wapenzi wa combat sports duniani; upande wa boxing kutakuwa na pambano kubwa linalomuhusisha bingwa na no1 P4P anayejulikana kwa jina la Saul Alvarez almaarufu kama Canelo ambaye ni mmexico, pamoja na mmarekani Caleb Plant ambaye pia ni bingwa katika uzito wa Super middleweight, hivyo watakuwa wakiunify mikanda yao na atakayeibuka mshindi atakuwa 'Undisputed Super Middleweight World Champion'. Pambano hilo la PPV linatarajia kuteka nyoyo za wapenda masumbwi duniani kutokana na amshaamsha zilizoanzia kwenye press conference yao ya kwanza.

UFC: kwenye upande wa Martial Arts kutakuwa na mapambano matatu ya kukata na shoka (PPV) ambayo yatakuwa headlined na wakali wawili wa Welterweight; Kamaru Usman (Mnaijeria) ambaye ndio Champion, na Colby Covington (Mmarekani) kama challenger. Wawili hawa wamewahi kukutana mara moja, pambano lao la kwanza lilikuwa mwakajana ambapo Usman alifanikiwa kuutetea mkanda wake, japo ilikuwa ni vita kali hadi Round ya mwisho Usman alipofanikiwa kushinda kwa TKO. Usman kwa sasa ndio no1 P4P kwa upande wa UFC, hivyo anapewa nafasi kubwa kuutetea mkanda wake.

Karibuni kwa updates hadi siku ya mapambano haya..

View attachment 1998607View attachment 1998608
Ungeanzisha uzi wa UFC ingekuwa poa sana [emoji91]
 
Back
Top Bottom