Figisu: Basi la Mamelodi la kuwapokea Yanga lasimama njiani na kuwaomba wasubiri litengenezwe, Yanga waamua kutumia hiace ndogo

Figisu: Basi la Mamelodi la kuwapokea Yanga lasimama njiani na kuwaomba wasubiri litengenezwe, Yanga waamua kutumia hiace ndogo

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760


Ni wazi kabisa hizi figisu ila cha kushangaa ni kuona timu kubwa kama Mamelodi kufanya hivi vitu wakati wao walipokelewa vizuri hapa Tanzania, tushazoea kwa waarabu ila sasa imeanza kuwa hadi kwa waafrika wenzetu?
 
Me sioni shida hapo, Hakuna asiepata dharula/hitilafu labda Mungu ndo sijui.
 
Vitu vya bure
Mikakati ya kuwaondoa mchezoni
 
Waziri wa michezo aliposema hakuna kushangilia upinzani (vita ya mdomo) watu wengi mlimpinga na wengine kudai ajiuzulu, sasa hawa wenzetu wao vita yao ni ya vitendo na unapasuka kweli bila kupigiwa kelele, unapasuka nje na ndani ya uwanja.
 
Hayo ni mambo ya kawaida sana kwenye soka barani Afrika. Timu nyingi zimeshazoea hali hiyo ndiyo maana zimeacha kutumia huduma za bure kutoka kwa wenyeji wa mechi.
 
Hiyo ni dalili ya hofu tu, kuharibika bus ni mpango wa Mamelodi kuwatoa Yanga mchezoni ila binafsi naona droo ya goli moja moja inamaliza Safari ya Mamelodi.

Yanga wasifunguke, wakabie juu kwa nguvu kwa dkk tisini ili kutotoa nafasi ya Mamelodi kucheza kwa utulivu na goli la Yanga litakuja lenyewe kwa counter attack ya Max Nzengeli.

All the Best Yanga , daima mbele
 
Hii ni fitna ya wazi sababu inaonesha gari haikufanyiwa ukaguzi kabla ili kujua usalama wake
Wote tunajua chombo Cha usafiri hasa bus tena kubwa la hivyo hukaguliwa kabla ya kutumika
Hii ni vita na ndio kitu si tunapenda Mamelody atachakazwa vibaya mno hapo loftus mbinu aliyotumia ni old fashion Gamond hajapenda hata kibabage nimeona kachukizwa kazi wanayo
 
Inatia shaka kwa timu kubwa yenye bajeti kubwa kama Mamelodi kuwa na mabasi yenye hitilafu
Hiki ni kiwango cha juu cha ujinga, Mamelodi inamiliki Car hires?

Hivi Yanga wakienda Avis car au kampuni yoyote inayokodisha magari ikawapa wageni wake, lile gari ikipata itilafu utasema Yanga ndio tatizo?

Kichwa kisichokuwa na akili ni mzigo Kwa shingo.
 
Waache watutie hasira ili ijumaa tuwakande vizuri!! 💛💚
 
Acha Yanga yateseke yanataka kudeka deka kila mahali
Hakuna sehemu Yanga itateseka, hii mechi Yanga anacheza kama Yuko nyumbani tu nyomi la kutosha.

Kama upo Johannesburg njoo hapa Rosebank nikupe ticket bure.
 

Attachments

  • FB_IMG_1712078859307.jpg
    FB_IMG_1712078859307.jpg
    89.2 KB · Views: 1
Back
Top Bottom