Figo zimefeli ghafa umri miaka 37

malembeka18

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2018
Posts
3,266
Reaction score
3,698
Habar wakuu..nimerudi kuomba msaada kwenu.. nna ndugu yangu jinsia ya kiume jana majibu yameonesha figo zake zimefeli zote.

Ni hivi huyu ndugu yangu ameanza kujiskia vibaya tangu majuzi kazidiwa akapelekwa hospital akakutwa na presha 220/105 na hajawahi kuugua presha..... wakamreferal MNH, baada ya kufanyiwa vipimo akabainika kuwa figo zote mbili zimefeli.

Wakuu, je presha ya ghafla inaweza sababisha figo kufeli na vipi matibabu yake uwezekano wa kupona!
 
Poleni sana mkuu ni kweli Presha ikipanda kwa kiwango hiko inaweza kusababisha Moyo, Figo kufeli na hasa kama alikuwa hajui juu ya Presha hiyo kuwa juu maana yake hata dawa hakuwa anatumia.

Matibabu yake ni Dialysis na Madaktari wakiona inahitajika kubadilishwa figo basi mtaambiwa.
 
Wakuu je wakuu presha ya gafla inaweza sababisha figo kufeli na vipi matibabu yake uwezekano wakupona

Renal failure inaweza ikapelekea mtu akawa na shinikizo la damu, na kinyume chake pia ni hivyo hivyo...

Hospitali watakuwa wamewapa majibu kujua sababu inayoweza kuwa chanzo cha figo kufeli au kuwa na ongezeko la ghafla la shinikizo la damu...
 
Mkuu pole sana nitafute mimi kwa wakati wako ili niweze kukutibia uapte kupona amradhi yako uguwa pole
 
Hypertension inayopelekea renal failure tena bilateral sio kawaida kutokea kwenye umri wa miaka 37, inawezekana kuna secondary cause ambayo sisi humu kwenye forum hatuijui..

Ila kikawaida kukiwa na shinikizo kubwa la damu, kiungo kinachoanza kuathirika ni figo kwa kuwa figo ni kiungo kinachodekezwa na kupendelewa sana mwilini, hebu fikiria katika kila msukumo mmoja wa damu unaotoka moyoni kwenda kwenye systemic circulation, 65% yote inaenda kwenye figo!

Btw, mgonjwa yeyote mwenye renal failure matibabu yake ni dialysis, renal transplantation watafanya endapo atapatikana HLA matched donor.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…