philosophy
Senior Member
- Nov 11, 2012
- 104
- 42
Mwanabusara Leopord Senghor na rais wa kwanza wa Senegal aliwahi kumtetea mwafrika kutoka maono baguzi ya uweupe akasema kuwa, " waafrika wana akili kama watu wengine, wanafikiri vizuri na wanautumia vema ufikiri huo kutoka ktk kiini cha urazini wao. Ila utofauti wao ktk kufikiri na wazungu ni kuwa hisia au mvuvumko wa hisia nao ni sehemu pia ya kufikiri kwa mwafrika. Hi yo ni njia nyingine ya kufikiri kwa mwafrika." Kwa hiyo kufikiri huko huambatana zaidi na mguso wa ndani wa mtu ambapo mwafrika hueleza hisia zake km sehemu ya fikra na ufahamu wake.
Wapo baadhi ambao walimwelewa zaidi kuhisia bwana Senghor na hivyo kudhihirisha maneno yake. Na hao walikuwa wa kwanza kumpinga au kumkosoa kwa msukumo wa uvuvumko wa kihisia pia pasi kutafakari hilo, na hakika bila wao kujua kumbe kukataa kwo kwa hisia bado walikuwa wanampa umashuri mwanafalsafa huyo.
Senghor yawezekana aliona mbali sana kulko sisi. Niliendelea kufatilia na kufanya uchunguzi na utafiti wangu taratibu. Kwa uhakika nikadhihirisha na ninazidi kushawishika wazi kuwa sisi waafrika tunatumia sana hisia kuliko tafakuri japo Senghor yeye anatetea km mfumo murua wa kufikiri. Mimi ninamuunga mkono kwa kusema tunafikiri kwa hisia ila nampinga kwa kusema hisia ni njia ya kufikiri. Kwangu mimi, hisia sio kufikiri bali ni mapungufu ya ufikiri. Hisia huwa hazimfanyi mtu atafakari au ahoji ukiini wa tatizo na udhabiti wa jambo lenyewe. Kuhisia jambo na kulitolea maamuzi kwa msukumo wa joto la hisia ni kukurupuka na wala sio kutafakari.
Ukweli huu nimudhibitisha leo wakati nilipokutana na marafiki wawili wakibishana na hadi kuchukiana kwa sababu mmoja wao alitamka neno ambalo kulingana na muktadha wa mazungumzo na ushahidi unaohitimisha hoja ile kwa mujibu wa mtazamo wake lile neno lisingehepukika. Kutokana na kutokuelewa au kufikiri kwa kina juu ya matumizi ya neno hilo, rafiki mwenza akamjia juu na kumchukia kwa kudai ati yule rafiki kamtukana kumbe sivyo bali huyu kafasili kinyume neno hilo. Nilpopata kuyatafakari maelezo yao wote nikabaini huyo rafiki aliyeng'aka alikurupuka kwa mchocheo wa hisia kali pasi kufikiri na kujua maana na kwanini mwenzie alitamka vile.
Oh, nkamkumbuka Senghor na nikaanza kuupata ukweli wake. Hizo ni hisia tu.