Fikiri Kuwa Sayari Tunayoishi ( Dunia) Ni Jehanamu Ya Sayari Nyingine...!

Fikiri Kuwa Sayari Tunayoishi ( Dunia) Ni Jehanamu Ya Sayari Nyingine...!

Ni kazi kubwa sana binadamu kujua ukweli ulioko kwenye ujinga tunaoufanya
Nashindwa kujua sababu ya watu kuhusisha thread hii na siasa
Inawezekana sisi ni wavivu wa kufikiri kuliko tunavyodhani!
 
Kwahiyo jehannam yadunia ita kuwa sayari gani? Maana shetani kesha sema dunia inaaisha 20. 12. 2012
 
Ndugu zangu,

Kwamba kuna viumbe kwenye sayari nyingine wenye kukesha wakiomba kwenye nyumba zao za ibada, kuwa Mungu wao awaepushe na balaa la kuwaleta kwenye sayari dunia.

Dunia iliyo zaidi ya tambala bovu. Dunia iliyojaa wanadamu wenye roho za wivu, kinyongo, inda, husda na nyinginezo. Wanadamu wenye kutakiana mabaya badala ya mema.

Na mfano ni huyu aliyeomba sana kwa Mungu ashushiwe rehma. Siku moja akashukiwa na malaika. Akaambiwa, kuwa Mungu amepokea maombi yake. Kwamba anamtaka mwanadamu huyu achague jambo moja ili ashushiwe. Na akishachagua moja, basi, Mungu atampa jirani yake mara mbili ya kitu alichochagua.

Mwanadamu yule akamwambia malaika; " Basi, niache kwanza nitafakari".

Baada ya kutafakari kwa muda,mwanadamu yule akatamka; " Namwomba Mungu anipe chongo!"

Kwamba kwa vile alimwonea kinyongo jirani yake apate mara mbili ya atakachokipata, mwanadamu yule aliona ni heri Mungu amtoboe jicho lake moja, awe chongo, na jirani yake atobolewe mawili, awe kipofu!

Naam, fikiri kuwa sayari tunayoishi yaweza ni jehenamu ya sayari nyingine.

Kumbuka, nimesema fikiri, hivyo basi fikiri kwa bidii...yaweza kukusaidia kupata jibu la kwanini nchi yetu ni masikini, na watu wake pia.

Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa

Idea za Kwenye Ben 10 hizo!
 
Huwa tunaishi kwa vile tuviaminivyo,ukiamini hii ni mbingu basi maisha yatakuwa kama mbingu vivo hivo kwa jehannum
 
narejea wanasayansi wawili maarufu duniani, mmoja ni darwin na mwingine ni Carl max. darwin alisema viumbe vyote duniani vinashindana katika kuweza kuishi na vile vyenye nguvu vitaishi na vile vidhaifu vitaondoshwa. carl max alisema dunia yetu imetawaliwa na ugomvi(conflict) aliitazama dunia kama sehemu ya machafuko na ghasia, hakuona kama ina majadiliano ama makubaliano. hivyo kila kila binadamu au tabaka la watu lipo katika ugomvi.na dunia haiwezi kuendelea bila ugomvi. alisema pia ''conflict is an engine of social change'' and once a conflict is resolved then another one bigger emerged. nikiwatafakari hawa watu wawili napata picha dunia sio jehanum kama tutaweza kuwa responsive to change.haaiitaji uwe geneous aau una misuli yenye nguvu au jeshi kubwa la vita bali ikiwa utaweza kubadilika kuendana na mabadiliko utaweza ku-survive. hata nchi yetu kama tutakuwa na viongozi wenye vision na wakaweza kuendana na mabadiliko ya kiulimwengu tutauaga ila kwakuwa viongozi tuliowachagua ni 'vimeo' inatupa shida. mfano; USSR walikua na jeshi kubwa lakini hawakubadilika wakaishia wakawaacha Nato ikitamba ulimwenguni. hata marekani ilikuwa iishie lakini kwa kuingia obama na kuhubiri 'change' wameweza kuwepo hadi leo hii wao ni super power ulimwenguni
 
Back
Top Bottom