Fikiria kila mtu ni msaliti ila hajagundulika tu,hii itakusaidia kupunguza mshtuko endapo mambo yakienda vibaya

Fikiria kila mtu ni msaliti ila hajagundulika tu,hii itakusaidia kupunguza mshtuko endapo mambo yakienda vibaya

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Wale ambao mnatembelea mitandao mbali mbali,kuna habar huko katika ule mtandao wa kindege,kwamba kuna mwamba ambaye yupo karibu na mkuu wa kaya,huyu mwamba kamnunulia tamu yake apartments kadhaa,na kila mwezi humpa milioni ishirini (20ml) za matumizi tu.

Sasa ebu fikiria,tamu ya mwamba pamoja na kuhongwa apartments na pesa mingi kila mwezi lakini kamsaliti mwamba mwenye fedha zake mjini,je wewe ni nani usisalitiwe?

Kwahiyo ukitafakar kwa akili huru hakika utajua kuwa usaliti ni mwingi mno katika mahusiano yetu na ndoa zetu,ni vile hujagundua tu bado,au labda mda wa kujua haujafika bado.

Kwahiyo njia bora ya kufanya ili hata haya mambo yatakapo kutokea usiathirike sana ni kuingiza akilini mwako kwamba lolote laweza kutokea kwa huyu mpendwa wangu.

Usimchukulie ni mtakatifu sana au mwaminifu sana au msafi sana,ukifanya hivyo rafiki yangu ndiyo yanakuja yale ya kutaka kujitundika na kujifanya wewe ni Mkwawa,na kuanza kulialia ooh nilimwamini sana mara sikudhani kama angenisaliti na blablabla kibao

Haya mambo huwa hayana muamana,lolote laweza tokea mda wowote ule,haijalishi una honga nyumba au magari,walisema wahenga hakika moyo wa mtu ni kichaka,kwahiyo kaa kwa kutulia

Kikubwa omba uheshimiwe na kupendwa na mwenza wako,hilo ndio jambo kubwa na shukuru kwa hilo lakini usitake kutafuta yaliyo fichikana bali acha yajifichue yenyewe mtu wangu

Sisi ambao shughuli zetu hutufanya tutoke mji mmoja na kwenda mwingine tunaona mengi,unakuta mwamba anakuwa na tamu yake kwa mda fulani halafu mke au mpenzi wake akija kumtembelea,yule side chick / kimada wake anasepa kwa muda,halafu baadae hali ya hewa ikiwa nzur anarudi kwa mwamba na ratiba zinaendelea

Mwanamke nae hivyo hivyo,akitembelewa na mtu wake au ubani wake basi mkunaji wake nae anasepa halafu mambo yakiwa sawa,mambo mengine huendelea

Kwahiyo usaliti ni mwingi sana tena kwa wale ambao wanakaa miji mbali mbali,ni wachache sana huwa waaminifu tena wachache sana,kwahiyo kikubwa kwakuwa hujui ukweli wa mambo basi wewe jenga tu uaminifu kwa mwenza wako,lakini weka akiba kwamba lolote laweza kutokea,itakusaidia walau maumivu yasiwe makubwa sana pale itapo bainika

Wanaume wenzangu chukueni hii,usikubali ujinga wa kuambiwa na tamu yako kwamba "babe ujue huyu rafiki yako ananitaka au mtu fulani ananisumbua ila mi namkataa ila yeye haelewe tu" anaweza kwenda mbele zaidi na kukuonyesha hata meseji za mwamba,shtuka boss,mara nyingi huwa ni defensive mechanism tu,lkn tambua asilimia kubwa huwa ameshaliwa

Ngoja nikupe kisa kimoja,kuna mwamba alikuwa anaambiwa na tamu yake hivyo hivyo"ooh babe ujue best yako fulani ananisumbua sana lkn mimi nishamwambia kuwa simtaki lkn haelewi" na meseji akawa anaonyeshwa,lahaula kumbe mungu si athumani,wakati anasoma meseji na tamu yake mara paap meseji kutoka kwa mtu huyo huyo ikaingia inasema "babe tutarudia game lini tena?" Nadhana unataka kujua ilikuwaje,acha ujinga


Kwahiyo usikubali kuambiwa na tamu yako habar hizo hata kidogo yan akianza tu mwambie sitaki kusikia huo ujinga,kuna mwamba mmoja huku aliandika uzi kuwa mwanamke wake anataka wahame kisa alipewa namba na jirani yake ambaye ana mke,kwanini uhame chumba kisa eti mwanaume wa jirani kamtumia mke wako namba yake ya simu,kwanini mke asiseme hataki mawasiliano na huyo mwanaume kwakuwa ana mtu wake,na badala yake anamshauri mume wake wahame,hapo kuna tatizo huenda ashaliwa tayar so anaona mwenye mume ashagundua huenda kikawaka mda wowote ule.

Narudia tena usimchukulie mume wako au mke wako kuwa ni mtakatifu na msafi sana,bali jua yeye ni binadamu na lolote laweza tokea katika maisha haya,kikubwa anakupenda na kukuheshimu na anakuthamini,usitafute yaliyo fichikana kwa kutrack simu yake au kupelelezana kwa namna yoyote ile utayakuta yasiyo kufurahisha.


Ni hayo tu!
 
Haya mambo huwa hayaeleweki na hayazoeeleki......jibu utalipata mpaka likikufika........

Huwezi kujua kama dunia ina mambo mpaka likukute jambo
Lkn mimi binafsi,likitokea la kutokea ntadili na mke wangu tu basi,yan haijalishi ntaumia kiasi gani,coz mwisho wa siku hakubakwa na huenda ilipochomoka akaiingiza tena

Huwa sina mambo mengi
 
Back
Top Bottom