FIKIRIA WEWE PIA NI MTU WA AINA GANI?

FIKIRIA WEWE PIA NI MTU WA AINA GANI?

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Kabla ya kuanza kuwalaumu wenzanko jiulize vyema wewe pia ni mtu wa aina gani , Je, wewe ni mtu wa aina gani unapo oneshwa upendo na wewe ni mtu wa aina gani unapo oneshwa chuki

Kabla ya kuanza kutoa majibu haraka penya ndani yako kisha ujiulize ikiwa ndiyo wewe ungesalitiwa ungekuwa mtu wa aina gani? iki wewe ndiyo ungeoneshwa dharau ungekuwa mtu wa aina gani?

Sisi ni wa aina gani pale tunapo yaunda maisha yetu ya kila siku, tunapata machaguo pale tunapo anza kujitafakari sisi ni wa aina gani?

Tunapo shindwa kujitafakari sisi ni wa aina gani huwa tunabebwa na kanuni mbovu sana katika kuhukumu.

Ukifahamu hata wewe ni wa aina gani utaona haina haja kushikilia hukumu za wengine kiwepesi, utaona haina haja kulaumu sana kwakua umepenya ndani ya Roho yako na kujiona wewe mwenyewe ulivyo si kimaoni bali kiuhalisia

Unachukia wengine kukusengenya je wewe husengenyi wenzanko iwa kwa kikundi au hata wewe binafsi .Jifikirie wewe binafsi unavyo fanya katika hali nyingine
 
Ni ngumu sana kujichunguza wewe mwenyewe ila ulichokisema ni ukweli
 
Unayozungumza yana ukwl ila sasa itategemea na Namba mtu anavyoutafsiri
 
Back
Top Bottom