Fikra pevu na adimu nchi hii

Seneta Wa Mtwiz

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2013
Posts
3,635
Reaction score
4,160
Na yeyote anayekosea japo namna ya kuushika hata awe nani, anapewa adhabu kali ambayo ni ngumu kuisahau na ni funzo kubwa kwa wengine (wakati huohuo).

Sa' usiku wa kuamkia leo nimejaribu kufikiria sana kuwa:

Je, ikitokea Rais amejichanganya siku ya kuzima mwenge kitaifa, akavaa kaptura yake nyeupe, yebo nyekundu na singlendi ya zambarau. Akaenda mbele ya umma, akaurukia mwenge, akaanza kucheza nao kiduku, kisha akauweka begani na kuanza kukata nao mauno kwa shangwe, nderemo, ubishi na hasira, huku matukio yanarushwa live na vituo mbalimbali vya televisheni nchini na nje.

Ikithibitika kuwa akili zake ni timamu na hana tatizo lolote la ubongo, hapo askari/wanajeshi watamfanya nini?

Nimewaza sana yani.
 
Tusubiri ikitokea tutapata jibu sahihi
 
A.c.t ya zito watasema kahamia chama chao kwa hizo jezi ulizotaja hapo
 
Uchizi sio lazima kuokota makopo, hata kufanya jambo la ajabu likawa kinyume na staha ya nafasi yako kwenye jamii ni ukichaa tosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…