Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 26,483
- 40,130
Awamu hii ya sita, hususan baada ya Rais Samia kumteua Wambura kuwa IGP, tumeshuhudia ukatili mkubwa tena wa wazi unaotekekezwa na polisi dhidi ya viongozi na wanachama wa CHADEMA.
Mara kadhaa tumeona viashiria vya uhusika wa Polisi kwenye utekaji, ulawiti, utesaji na hata vifo vya wanachama wa CHADEMA. Tumemsikia Msemaji wa Polisi akitetea kuwa wanachama wengi wa CHADEMA wamepotea kwa sababu za wivu wa kimapenzi, kudaiana na kulipizana visasi huku ikiendelea kutoa ahadi ya kufuatilia waliopotea chini ya uhusika wao.
Ikumbukwe, kijana SATIVA alitekwa na kuja kupatikana amejeruhiwa. Katika ushuhuda wake alimtaja Mkuu wa Upelelezi Kanda maalum ya Dar es Salaam ndugu Mafwele kuhusika na tukio lake. Lakini hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi yake.
Hivi karibuni, IGP Wambura ametoa onyo kuwa wananchi wanaotaka kuandamana hapo Oktoba 29 wachague kuhama nchi. Hili ni tishio la pili kutoka polisi ambapo wiki kadhaa zilizopita, Kamanda wa Kanda Maalum Dar afande Muliro alitamka kuwa mwananchi atakayeingia barabarani Oktoba 29 ajiandae kufa.
Chini ya IGP Wambura, tumeshuhudia Polisi wakifanya matukio yanayofanana kama ya kigaidi dhidi ya raia wanaoikosoa seerikali.
Chuki inayopandwa na matendo ya Polisi dhidi ya wanasiasa wa upinzani inaendelea kukua