Fikra Tunduizi: Ukatili wa Polisi dhidi ya CHADEMA unaashiria nini?

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,483
Reaction score
40,130
Awamu hii ya sita, hususan baada ya Rais Samia kumteua Wambura kuwa IGP, tumeshuhudia ukatili mkubwa tena wa wazi unaotekekezwa na polisi dhidi ya viongozi na wanachama wa CHADEMA.

Mara kadhaa tumeona viashiria vya uhusika wa Polisi kwenye utekaji, ulawiti, utesaji na hata vifo vya wanachama wa CHADEMA. Tumemsikia Msemaji wa Polisi akitetea kuwa wanachama wengi wa CHADEMA wamepotea kwa sababu za wivu wa kimapenzi, kudaiana na kulipizana visasi huku ikiendelea kutoa ahadi ya kufuatilia waliopotea chini ya uhusika wao.

Ikumbukwe, kijana SATIVA alitekwa na kuja kupatikana amejeruhiwa. Katika ushuhuda wake alimtaja Mkuu wa Upelelezi Kanda maalum ya Dar es Salaam ndugu Mafwele kuhusika na tukio lake. Lakini hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi yake.

Hivi karibuni, IGP Wambura ametoa onyo kuwa wananchi wanaotaka kuandamana hapo Oktoba 29 wachague kuhama nchi. Hili ni tishio la pili kutoka polisi ambapo wiki kadhaa zilizopita, Kamanda wa Kanda Maalum Dar afande Muliro alitamka kuwa mwananchi atakayeingia barabarani Oktoba 29 ajiandae kufa.

Chini ya IGP Wambura, tumeshuhudia Polisi wakifanya matukio yanayofanana kama ya kigaidi dhidi ya raia wanaoikosoa seerikali.

Chuki inayopandwa na matendo ya Polisi dhidi ya wanasiasa wa upinzani inaendelea kukua
 
CCM huchagua viongozi wa nchi waliokuwa wana chama wao, bila ya kuwa mwanachama wa ccm huwezi kupewa nafasi kubwa Tanzania hii.

Kama kuna kiongozi yeyote hajawahi kuwa mwana ccm na alihudumia serikalini naomba atajwe.
 
Mabilioni anayomiminiwa kwenye account yake na huyu chura kiziwi yamempofusha amekuwa msukule wa mama Abdul.
 
Niswala la muda tu , hii nguvu tunayoiona kwenye mitandao nikamakutandaza majani makavu ,ipo siku tu cheche itapatikana tena na hizi dharau zao aisee ngoma itawaka kimizuka hatutaamini
 
Mabilioni anayomiminiwa kwenye account yake na huyu chura kiziwi yamempofusha amekuwa msukule wa mama Abdul.
Atapata wapi muda wa kutumia hizo pesa?
1985 alikua form five iliyokua Mazengo sekondari, that is he was around 20 years by then, ongeza another 40 years, utapata he is 59/61 hapo. At 60 and above mwili umeanza kuchoka hupendi tena viwanja, nguvu pendwa simeanza kupotea, visukari, tezi dume etc vinakunyemelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…