Filamu na maigizo ya Hollywood yanaiharibu dunia

huyo Mungu alopinga ni Mungu huyu wa hao wazungu au Mungu wa kiafrika!?.
Kwanza unachopaswa tambua ili kusema kitu flani ni kibaya inabidi urudi kwenye mizizi kabisa na kuchimbua, sasa wewe unasema ustaarabu wa kuoana wakubwa na wadogo mbaya wakati huo unatumia Mungu wa kizungu, huoni unajicontradict!!..
Hutakiwi sema wazungu wametuletea utamaduni mbaya wakati Mungu unayemuamini na kumlilia ni wao pia, mkatae na yeye basi!.
 
Kwa hiyo yanayofanya kwenye filamu za Hollywood ni maagizo toka kwa mungu? Ndo maana inabidi tuyakubali. Naomba nikukumbushe Dunia hii ina upande wa giza sio kila kinachotokea kimeratibiwa na mungu kuna mipango ya kishetani (devil's work).. Turudi kwenye mizizi ni mizizi ya wapi iliyohalalisha niliyoyataja?
 
mzee hivi unajua sir godi kaipiga mara 2 dunia lakini wahuni hawajakoma!.
1. sir godi akashusha mvua dunia nzima (gharika kuu), kipindi hiko watu wanakula mpaka za mijusi!.
2. sir godi anaamua choma miji miwili yotee (sodoma na gomora) usifanye mchezo ujue!.
Wewe ni nani kuja sema sasa hivi maadili yamepungua wakati yapo ya kutosha!. Nakwambia ungezaliwa kipindi cha sodoma na gomora yanayofanyika saa hii ungesema hiiii hawa nao wanajikuta wamechafukwa!.πŸ˜‚
 
Mizizi ya tamaduni zao inakubali hayo yote!. Nionyeshe wapi inakataa!.
Nikupe tu kaidea, unajua biblia za zamani zilikuwa zinatengenezwa kwa kutumia karatasi zilizotokana na mjani wa bange!?
hivi ulishawahi fuatiria mtu anayejiita BABILONI kalitoa wapi hilo neno!?
nakwambia tena exposure inakusumbua!πŸ™‚
 
Kumbe unatambua jinsi gani mungu anachukizwa na vitendo viovu sasa kwa nini uone sawa yanayoonyeshwa kwenye filamu za Hollywood kama sio unafiki na uzandiki wa kiswahili.
 
Hongera kwa kuwa na exposure ya mambo hayo as long unaona upo sawa Mimi ni nani hasa mpaka nikuzie unachoamini
 
GOT dah kale ka-theme ka mwanzo kale dahhh
 
Kinachotafutwa na hao wenzetu ni kuunda utamaduni mmoja wa dunia utamaduni wenye uovu ambao kwa kipindi kirefu ulikuwa unafichwa ili kiifanya jamii iwe stable at least,
Nia yao ovu ya kuzifanya deviance culture kuwa juu na hata kuwa ndo kiigizo
 
Aisee hayo madudu yapo Kila mahala,
Kinachotakiwa ni wewe kujitambua na kucontrol akili yako pamoja na msimamo thabiti,
Ila nasikitika hawa watoto/vijana wa sasa hivi ambao ndio kizazi kijacho ndio watakao/wanaopotea,

Kama unajielewa na kujitambua lazima utakua unajua lipi baya, lipi zuri
Binafsi naangalia movie hayo madudu yao nawaaachie wenyewe,

Kila mtu ashike usukani wake apeleke gari yake eidha kwenye misumari au kwenye rami ikiharibika/isipoharibika ya kwake, hakuna haja ya kubishana/kulazimishana
Kama yako ni nzima na unajiona upo sahihi basi sawa, ishi kwenye ulimwengu wako unaoona unakufaa hayo mengine waachie wenyewe,

ukiona mtu anashawishika na Kila anachokiona hata kiwe kibaya na anajua ni kibaya basi lazima atakuwa mtoto Kama sio mtoto basi huyo mtu hajitambui,akili zake ndogo, anashikiwa akili.
WEWE ACHANA NAYE AMINI UNACHOONA UPO SAHIHI.
 
Game of thrones ilikuwa na tatizo gani? Ilikiwa na kitu gani ambacho ni cha ajabu sana ambacho duniani kilikuwa hakipo au hakijawahi kuonyeshwa?
Wanawake kujiuza? Ushoga na usagaji vilikuwa kwa kiasi kidogo sana
Kama vip tazama tu bongo movie,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…