Finance Bill 2026: Serikali Yalenga Mitumba, Simu na Magari — Je, Mwananchi wa Kawaida Ataumia Zaidi?

Finance Bill 2026: Serikali Yalenga Mitumba, Simu na Magari — Je, Mwananchi wa Kawaida Ataumia Zaidi?

OwadeKuya

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
535
Reaction score
312
Finance Bill 2026 imeleta mjadala mkali sana miongoni mwa Wakenya, especially kwa sababu inagusa vitu za everyday life kama mitumba, simu na hata juice. Serikali inasema hii ni njia ya kuongeza revenue, lakini wananchi wengi wanaona mzigo unaongezeka.

Kwa mfano, wafanyabiashara wa mitumba sasa watahitajika kulipa tax ya 5% ya value ya mzigo wao wakati wa ku-import. Hii ina maana bei ya nguo za bei nafuu inaweza kupanda — na kama unajua, mitumba ndio “uniform” ya wengi mtaani.

Pia kuna proposal ya 25% excise duty kwa simu, ambayo italipwa wakati wa activation. Hii inaweza kufanya smartphones kuwa expensive zaidi, kitu ambayo ina-affect especially vijana na biashara ndogo ndogo zinazotegemea online platforms.

Kwa upande wa magari, kuna excise duty ya 50% kwa vintage vehicles zenye value ya over KSh10 million. Hii inalenga more high-end buyers, lakini bado inaonyesha serikali inaangalia kila sector kuongeza mapato.
Kwa gamblers, serikali inapendekeza 20% tax kwa winnings — so ukibahatika kushinda, kumbuka serikali pia iko kwa hiyo deal. Scrap metal sellers nao wataanza kulipa 1.5% withholding tax.

Lakini si yote ni mabaya — kuna VAT exemptions kwa vitu kama electric buses, bicycles, na baadhi ya medical supplies. Hii inaweza kusaidia sectors kama transport na afya kukua.
Mabadiliko mengine muhimu ni deadline ya tax returns kuletwa mbele hadi April badala ya June, na wale wanafanya Nil returns watahitajika kufile mapema zaidi January.

Swali kubwa ni: Je, hizi changes zitasaidia uchumi kukua au zitazidi kubana mwananchi wa kawaida? Wengi wanaona kama hizi taxes zitapandisha gharama ya maisha, especially kwa wale already wanajitahidi ku-survive.

Kwa sasa, macho yote yako kwa Bunge kuona kama mapendekezo haya yatapitishwa au yatabadilishwa baada ya mjadala.

Wewe unaonaje? Hii Finance Bill ni relief ama ni pressure zaidi kwa mwananchi?

Source: Afrinews
 
Back
Top Bottom