Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asilimia 99.9 ya pesa za serikali zinazokwenda kwenye malipo ya "per diem" zinatokana na PESA ZA MISAADA KUTOKA WAFADHILI WA BAJETI YA SERIKALI KILA MWAKA! Kwa vile ni pesa za bure za Wazungu basi hakuna aliye na uchungu nazo na ndiyo maana kila mtu anahusika kutoka Waziri hadi tarishi ofisini. Kwa kifupi, uhusiano kati ya Serikali na Wafadhili kutoka Ulaya umeishia kuwa kama ule wa msichana na buzi lake.
Ukitaka kujua kifo chetu kama Taifa, angalia topic kama hii uone kama watu watachangia sana. No wonder, tunakesha JF kuandika badala ya kufanya kazi. Najivunia post zangu chache na muda mwingi wa kuchapa kazi. Wanafunzi, wanasiasa, usalama, wahadhiri, wapambe, n.k wanakesha humu halafu eti tutegemee maendeleo. Huo ni muujiza!
Mkuu hakuna pesa za bure hapa, hii yote tunayoita misaada ni mikopo na inchangia kwenye deni la taifa.
Kama kuna viongozi wanaofikiri kwamba misaada ya wafadhili ni pesa ya bure basi hawastahili kushikilia nyadhifa walizonazo!
Tunahitaji MAPINDUZI YA UTAMADUNI kuondokana na mfumo huu, Rwanda wameweza nasi tukipata uongozi wenye dhamira ya dhati hili linawezekana. Nakumbuka Raisi mstaafu BWM alilizungungumzia sana hili lakini hatukuona akichukua hatua kwa vitendo, labda wenzake hawakumpa ushirikiano.
Kwa maana nyingine posho ni un-fair distribution ya compensation ya government. Wanapata wachache wengi wanaachwa chini.
No wonder viongozi wakuu wanakubali malipo ya mil.4. maana eventually wanapata mil. 25 kwa mwezi.
Same same government total payroll and benefits...inaweza gawanywa vizuri na kufanya mfumo wa payment wa serikali uwe fair na u-promote efficiency.
Lakini wakubwa hawako tayari kuzungumzia hili hata kidogo.