Financial Times on 'Institutionalized Culture of Time Wasting & Per Diem' in Tanzania

hili ni tatizo kubwa sana,dawa ni kujipanga upya na kutengeneza sheria mpya kabisa kuhusiana na haya mambo la sivyo tumekwisha!
 
We are plagued by a pandemic poverty of mind, a systemic smallmindedness and a virulent vision that cannot vacate our visages.
 
Asilimia 99.9 ya pesa za serikali zinazokwenda kwenye malipo ya "per diem" zinatokana na PESA ZA MISAADA KUTOKA WAFADHILI WA BAJETI YA SERIKALI KILA MWAKA! Kwa vile ni pesa za bure za Wazungu basi hakuna aliye na uchungu nazo na ndiyo maana kila mtu anahusika kutoka Waziri hadi tarishi ofisini. Kwa kifupi, uhusiano kati ya Serikali na Wafadhili kutoka Ulaya umeishia kuwa kama ule wa msichana na buzi lake.

Nasubiri kwa hamu matokeo ya Uchaguzi mkuu wa Norway baadaye mwaka huu ambapo chama cha Progressive Party (Frp) kimeamua kusitisha misaada yote ya kimaendeleo kwa Serikali ya Tanzania.

Mtakumbuka skendo ya Wizara ya Mali Asili na Utalii mapema mwaka huu ambapo utapeli mkubwa uligundulika kuhusu pesa kibao za wafadhili kutoka Norway zilivyotumika kiholela kugharamia vikao, semina na "per diem" kwa wafanyakazi hewa wizarani.
 

Mkuu hakuna pesa za bure hapa, hii yote tunayoita misaada ni mikopo na inchangia kwenye deni la taifa.

Kama kuna viongozi wanaofikiri kwamba misaada ya wafadhili ni pesa ya bure basi hawastahili kushikilia nyadhifa walizonazo!

Tunahitaji MAPINDUZI YA UTAMADUNI kuondokana na mfumo huu, Rwanda wameweza nasi tukipata uongozi wenye dhamira ya dhati hili linawezekana. Nakumbuka Raisi mstaafu BWM alilizungungumzia sana hili lakini hatukuona akichukua hatua kwa vitendo, labda wenzake hawakumpa ushirikiano.
 

JF imeanza lini na umasikini wa Watanzania umeanza lini?? Mjaribu kutoa hoja zenye mashiko, huwezi kulipuka tu na kusema JF inawafanya watu wawe wavivu ili hali wanauhabarisha na kuuelimisha umma. Wewe kama ni mvivu wa kutoa maoni humu jamvini, huo ni ufisadi mwingine kwa sababu kama unajambo la kuielimisha jamii huwezi kukaa nalo na mkeo/mmeo alafu useme unatimiza wajibu wako ktk jamii. Hata kutowatendea haki watoto, wazee, n.k. ni ufisadi tu.
 

Jamani hiyo Rwanda mnaosema wameweza wameweza lipi zaidi?? Mbona sisi tuna nafasi ya kufanya vizuri kuliko nchi zote EAC? sema tunakosa uongozi wenye vision na mission zinazo tekelezeka.

Ni kweli kwamba Rwanda wamejaribu hasa ktk sekta ya afya kuwalipa vizuri watumishi ili kuongeza molali wa kazi, hili TZ linawezekana si kwamba tunashindwa sema tu CCM hawataki kufanya.

Tanzania tukipata kiongozi mwenye maono kama Magufuli (tukiachana na issue ya uuzwaji wa nyumba) basi tunaweza kupiga hatua. Vinginevyo tunahitaji chama mbadala ili kuleta maendeleo ya kweli.
 

wenyewe watakuambia kuwa na wage bill huge huwezi ku justify maana kazi zifanywazo siyo nyingi ki hivyo....mfanyakazi wa serikali output yake ni ndogo.... kazi inayoweza kufanywa na mtu mmoja hufanywa na msururu wa watu...
njia nyingine ni kuwapunguza watu kazini...lakini huku ni kuwatupa wananchi kwenye ufukara zaidi....
la per diem..... hili linaumiza watu vichwa sana hasa wafadhili lakini hakuna namna....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…