"Fine and Sexy" Bungeni! Mbunge Millie Odhiambo ametetea Passaris, Junet ahoji kauli hiyo

"Fine and Sexy" Bungeni! Mbunge Millie Odhiambo ametetea Passaris, Junet ahoji kauli hiyo

Wakaguongo

Member
Joined
Sep 23, 2026
Posts
95
Reaction score
38
Mvutano ulizuka katika Bunge la Kitaifa baada ya Mbunge wa Suba North Millie Odhiambo na mwenzake wa Suna East Junet Mohammed kutofautiana kuhusu matumizi ya neno "sexy" kumwelezea Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Nairobi Esther Passaris, aliyeadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya miaka 62.


Mabadilishano hayo yalitokea Jumatano, Oktoba 21, 2026, wakati wa mjadala kuhusu Mswada wa Harm Reduction uliowasilishwa na Passaris mwenyewe.

Katika mjadala huo, Millie alimtetea Passaris dhidi ya mitazamo inayowakejeli wanawake kutokana na umri wao, akisisitiza kuwa mwanamke anaweza kuendelea kuwa na mvuto, kujiamini na kujipenda hata anapozeeka. Millie alizungumzia namna Passaris anavyojipamba, anavyovalia na kujiwasilisha hadharani, akipinga tabia ya jamii kuwahukumu wanawake kwa umri wao au mwonekano wao.Hata hivyo, Mheshimiwa Junet alihoji matumizi ya lugha hiyo ndani ya Bunge, jambo lililochangia mvutano kati yao.

Tukio hilo limeibua mjadala mpana kuhusu namna wanawake wanavyotazamwa wanapozeeka, hasa wale walio katika uongozi wa umma. Wakati baadhi ya watu wanaweza kuona kauli ya Millie kama utetezi wa haki ya mwanamke kujieleza na kujithamini, wengine wanaweza kujiuliza kuhusu mipaka ya lugha inayofaa kutumika katika mijadala ya Bunge.

Je, jamii huwa na viwango tofauti vya kuwahukumu wanawake na wanaume wanapozeeka au Junet alikuwa na hoja kuhusu lugha inayopaswa kutumika ndani ya Bunge? Wewe unaonaje kuskia neno "sexy" ndani ya Bunge la Kitaifa?
 
Back
Top Bottom