Finland yatajwa kuwa Nchi yenye furaha zaidi Duniani

Finland yatajwa kuwa Nchi yenye furaha zaidi Duniani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Je, Wajua?

Finland ndiyo nchi yenye kiwango kikubwa zaidi cha furaha duniani kwa mujibu wa ripoti ya furaha ya Dunia ya Umoja wa Mataifa kwa miaka 7 mfululizo (2024, 2023, 2022, 2021, 2020, 2019, 2018).

Raia wa Finland wameridhika sana na maisha yao ya kila siku, jambo linalochangiwa na mfumo wa kijamii wenye uwiano mzuri kati ya kazi na maisha binafsi, huduma bora za afya na elimu, pamoja na mshikamano wa kijamii.

Moja ya sababu kuu ya furaha yao ni mazingira safi, nchi hiyo ina hewa safi zaidi duniani na maji ya kunywa yaliyo safi kabisa, hali inayochangia afya njema kwa wananchi wake.

1747727887180.png
 
Kudanganyana tu. Kuna nchi yoyote duniani yenye baridi kali watu wana furaha???
 
Ila nchi hii ina ubaguzi kiwango cha juu sana waafrica si mahali pazuri kwao utakufa kwa depression tu
 
Wao wanafurahia nini?

Huku tunafurahia pombe na kiti moto.
 
Back
Top Bottom