Zitto ni mgeni katika siasa ,anakumbuka Maalim Seif alipomwambia Kikwete kuwa ni mdogo kwake ,akimaanisha akimaanisha kisiasa, Zitto afahamu kuwa kama anataka kujiweka katika upande wa upinzani basi akae na wapinzani asikubali kwa hali yeyote ile hata kama jambo lina manufaa kwa Taifa kisiasa litamwangusha tu hana ujanja ,na ndio kama tunavyoanza kuona ,na ndio matamanio ya CCM ,watamtumia kisha watamtupa ,na kumpa kazi kama ya Tambwe hiza.
Katika siasa mara nyingi huwa nasema kuwa usijaribu kuiunga mkono serikali iliyoko madarakani hata kwa jambo la ukweli ,kwa vyovyote vile utafute propaganda zozote ulipinge juu chini uligeuze jambo lolote la serikali na kulitia ila mbele ya macho ya wananchi ,jamani ndio pakaitwa upinzani ,hawa akina maali Seif wamelalamikiwa sana juu ya kuipongeza serikali na vyombo vyake vya dola ,na siku hizi wamekaa sawa.
Maana kwa kila watakalolitenda serikali hii mbovu iliyojaa ubabaisha ,unaweza kuwapinga na kuwatia ila kwa jambo lolote lile watakalolifanya hata liwe la kweli ,maana serikali ikisema Mtwara kuna mikoroshi mingi upinzani unatakiwa useme serikali inasema uongo Mtwara hakuna mikoroshi kuna magogo tu ,au serikali ikisema Tanga kuna mkonge mwingi upinzani unatakiwa useme hakuna mkonge kuna msitu wa miba tu ,natumai nimeeleweka.