First date: Ya kufanya na ambayo hupaswi kufanya kwenye mtoko wa kwanza

Pure_sapiens

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2016
Posts
2,228
Reaction score
2,064
Habari za weekend wana chitchat.Huu uzi ni wa kushauriana mambo ambayo hutakiwa kufanya kwenye first date na Yale ambayo ni mazuri unayopaswa kufanya kwenye first date.
Mtoko wa kwanza ni siku ya kufanya tathimini kwa yule una mdate au siku ya kujenga profile.
First date ndio inatowa majibu ya kuwa nawe ama laaa hivyo hii ni siku muhimu sana.
 
Nilikurupuka nikajua ushayaeleza madude yote kumbe magumashi we jamaa hufai
 
Unapaswa kufanya:

1. Zingatia muda.

2. Vaa vizuri, tokelezea nadhifu.

3. Chagua eneo la kukutana sahihi, siyo mafichoni. Sehemu ya wazi inapendeza zaidi.

4. Jaribu kua mkarimu na mstaarbu.

5. Jaribu kua mkweli, na mambo utakayongea yawe sahihi na uwe na uhakika nayo.


Hupaswi kufanya:

1. Kujiongelea kuhusu wewe, kujikweza na kutokumpa nafasi mwenzako kuongea chochote.

2. Kuongelea mipango yako au yenu siku ya kwanza. Mara utamfanyia hiki, hiki na kile, utampa hiki, hiki na kile. Usitengeneze matumaini makubwa ambayo unajua hutokuja kuyatekeleza.

3. Usiongolee kuhusu mapenzi yako yaliopita au watu uliyokwisha date nao.

4. Usimpangie mkutane kwako au getto kwako.

5. Usioneshe ubinfasi.

6. Usizungumzie ngono. Kama ipo, ipo tu.


Cc: mahondaw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…