First year 2023/2024 elimu ya juu

First year 2023/2024 elimu ya juu

Rasasem

Senior Member
Joined
Jun 25, 2022
Posts
100
Reaction score
79
Habari wandugu, napenda kujumuika na ndugu zangu wote ambao wanaingia mwaka wa kwanza wa masomo 2023/2024 katika vyuo vyote tupeane mawazo, ushauri na tusaidizane changamoto zetu, ni njema pia kama ikipendeza hata kutujuza chuo ulichochaguliwa unaweza kupata rafiki mkaanza maisha mapya!

Wakubwa wetu pia tupeni msingi mzuri (ushauri) wa namna bora itakayotufanya tusome Kwa tija tukiwa vyuoni, kipi tuache na kipi Tufanye na si vibaya mkitupa changamoto zenu mlizowahi kupitia ili tujifunze!

Mimi nimechaguliwa UDSM@

Karibuni sana@
 
Mkiwa chuoni mjitahidi kutumia vizuri boom lenu hasa hasa mnaotoka kwenye familia zenye uwezo wa chini na kati ili msiendelee kuwatesa wazazi au walezi wenu. All in all ukiwa chuo kikuuu usiwe antisocial kumbuka watu wanaokuzunguka hapo chuoni ndo watakuja kuwa msaada wako baadaye. Heshimu kila mtu pia jichanganye na watu wote.
 
Ubarikiwe sana, tumepokea na tunashukuru mkuu🙏🙏🙏
 
Jitahidi usome vitabu Kama kiingereza kinakusumbua hakikisha unajua kiingereza vizuri , jifunze computer, jifunze kuendesha gari

Kaa mbali na wanawake hasa Hawa wanafunzi Wenzako ambao hawana exposure na Maisha .

Jitahidi kanisani wakujue hii itakufanya kuwa mtu wa kutafakari MAFANIKIO yako na ukuu wa Mungu.

Chuoni Zama hizi Kuna watu wachovu wengi so kaa nao mbali hasa watu wanopenda kuongelea habari za udaku ,wasanii, Simba na yanga ,habari za mademu nk.

Tumia muda wako kusoma Sana vitabu hapa simaanishi vitabu vya darasani
 
Epuka kuwa miongoni mwa zimamoto ,nitakuja kufafanua baadae faida na hasara za Zimamoto.
 
Jitahidi usome vitabu Kama kiingereza kinakusumbua hakikisha unajua kiingereza vizuri , jifunze computer, jifunze kuendesha gari

Kaa mbali na wanawake hasa Hawa wanafunzi Wenzako ambao hawana exposure na Maisha .

Jitahidi kanisani wakujue hii itakufanya kuwa mtu wa kutafakari MAFANIKIO yako na ukuu wa Mungu.

Chuoni Zama hizi Kuna watu wachovu wengi so kaa nao mbali hasa watu wanopenda kuongelea habari za udaku ,wasanii, Simba na yanga ,habari za mademu nk.

Tumia muda wako kusoma Sana vitabu hapa simaanishi vitabu vya darasani
Ahsante sana boss
 
Hii imenifanya nikumbuke miaka ya nyuma 2006 kuna jamaa yangu tulisoma nae alikuwa kipanga kwelikweli tangu form 1 mpaka 6 na alipasua vilivyo kwenye mitihani

Tulipoingia hapo UDSM na boom la kutosha jamaa alijichanganya sana akasahau yuko hapo anasoma engineering. Alistareheka vya kutosha ila hakutoboa hata mwaka alidisco kimasihara kabisa mpaka leo yuko mtaani anahaso sana.

Wadogo zangu furahieni maisha ya chuo(kula bata kiaina) lakini kumbukeni kilichowapeleka huko. hakikisha unajiwekea mazingira ya kutopata SUP, epuka kujifanya mjuaji na kumbuka pia ulikotoka.
Hongereni na kila la heri.
 
Asante sana bro
 
Kwahy story ni zile zile kila waliokua vipanga wakienda chuo wanaanguka
 
Hii imenifanya nikumbuke miaka ya nyuma 2006 kuna jamaa yangu tulisoma nae alikuwa kipanga kwelikweli tangu form 1 mpaka 6 na alipasua vilivyo kwenye mitihani

Tulipoingia hapo UDSM na boom la kutosha jamaa alijichanganya sana akasahau yuko hapo anasoma engineering. Alistareheka vya kutosha ila hakutoboa hata mwaka alidisco kimasihara kabisa mpaka leo yuko mtaani anahaso sana.

Wadogo zangu furahieni maisha ya chuo(kula bata kiaina) lakini kumbukeni kilichowapeleka huko. hakikisha unajiwekea mazingira ya kutopata SUP, epuka kujifanya mjuaji na kumbuka pia ulikotoka.
Hongereni na kila la heri.
Nikikumbk uliosema..... Angalia ulipotoka kipind naaga kurudi shule au chuo nilikuwa na feel kitu....

Alhamdullilah nilipita kote na nimemalza.
 
Habari wandugu, napenda kujumuika na ndugu zangu wote ambao wanaingia mwaka wa kwanza wa masomo 2023/2024 katika vyuo vyote tupeane mawazo, ushauri na tusaidizane changamoto zetu, ni njema pia kama ikipendeza hata kutujuza chuo ulichochaguliwa unaweza kupata rafiki mkaanza maisha mapya!

Wakubwa wetu pia tupeni msingi mzuri (ushauri) wa namna bora itakayotufanya tusome Kwa tija tukiwa vyuoni, kipi tuache na kipi Tufanye na si vibaya mkitupa changamoto zenu mlizowahi kupitia ili tujifunze!

Mimi nimechaguliwa UDSM@

Karibuni sana@
Chuo Kuna mengii.......

Jitahdii kusoma kwa bidii, fanya assignment, hudhuria vipind, fanya test na ue, accordingly km huna sababu ya special.

Tengeneza network nzurii na marafk, ukiwa chuon itakusaidia mbelen.....

Kufurahia maisha napo sio mbaya usijitese kisa upo chuo.... Kuwa na mipaka tuu.

Salii au amini ktk unachoaminii.....

Usome ufaulu sup sio nzurii..... Mdg angu
 
Back
Top Bottom