Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Niwapongeze wote mloweza kuchaguliwa Chuo kikuu cha dodoma,ni nafasi ya pekee kwani kipindi hiki kumekuwa na ushindani mkubwa wa kupata nafasi vyuon hasa vyuo vya serikali kutokana na mazingira,ada,ubora wa elimu n.k!mimi nitakuwepo mjengoni pale college ya informatics kupiga "bachelor of science in telecommunication engineering".
karibuni tufahamiane wakuu.
Jaman msaada et unapoenda kulipia ada benki pale kwenye payment slip sehemu ya jina unaandika jina ambalo lipo kwenye admission letter au unaandika uliyokuwa unatumia kidato cha nne
Niwapongeze wote mloweza kuchaguliwa Chuo kikuu cha dodoma,ni nafasi ya pekee kwani kipindi hiki kumekuwa na ushindani mkubwa wa kupata nafasi vyuon hasa vyuo vya serikali kutokana na mazingira,ada,ubora wa elimu n.k!
Kama mwanafunzi mwenzenu (4th year,Bsc Petroleum engineering) nilowatangulia ni vyema kuwapa ushauri/mwanga kidogo kabla hamjaripoti na kuanza masomo.
"UDOM" ni chuo kichanga ambacho kinaendelea kukua kadri siku zinavyokwenda,Kuna changamoto nyingi zinazokikabili chuo ambazo kwa asilimia kubwa zimepungua kwani chuo kilivyo kwasasa ni tofauti na kipindi kinaanza.Hata sifa mbaya zilizokuwepo miaka ya nyuma kwasasa hazipo tena,imekuwa ni moja ya kimbilio kubwa la wanafunzi kuomba nafasi.
Nini cha kufanya uweze kuzikabili changamoto zilizopo
1.KUSOMA KWA BIDII
Kumbuka jambo la msingi linalokupeleka chuo ni kusoma hivo jitahidi sana kusoma kwa bidii.Chuo kina ukosefu mkubwa wa "lecturers" hasa kwa kozi za sayansi(engineering) hivyo juhudi binafsi inahitajika sana kuhakikisha unasoma vitabu vingi,tumia sana mtandao kwa lengo la kujifunza.
Uzuri wa chuo mwalimu(lecturers) anakupa "course content" ambayo inaonyesha "topics" zote unazotakiwa kuzisoma katika kila "semester" hivyo ni vyema kuhakikisha unaipitia,chochote ambacho mwalimu hakukifundisha/hukukielewa vizuri unatafuta vitabu zaid uweze kuelewa!Kumbuka mwalimu anakupa 25% ilobaki ni jukumu lako,usiishie kusoma "notes",vitini vya mwalimu tu!
Ubora wa mwanafunzi pindi umalizapo chuo hutokana na wewe mwenyewe kujibidiisha kumlaumu mwalimu au chuo hakutakusaidia
2.JINSI YA KUISHI CHUONI
Tofauti na ulivyokuwa sekondari,chuon mtu uko huru kufanya lolote hakuna wa kukuonya!Hivyo ni vyema kuhakikisha unafwata kilichokupeleka pale achana na makundi mabaya,starehe na mambo mengine ambayo yanaweza yakakufanya ukashindwa kumaliza chuo(ku disco) au kumaliza chuo na matokeo mabaya!
Uzuri wa UDOM wanafunzi wote mnaishi ndani ya hostel za chuo na chuo kimejitenga kidogo na mji hivyo una mda mzuri wa kusoma na kujichanganya na wenzako kusoma pamoja!Tena ni vizur zaid ukimaliza usajili wakat wa kupewa chumba uishi na wanafunzi walokutangulia mwaka(2,3,4,5) uweze kupata ushauri kutoka kwako kwani wanakuwa na uzoefu zaid ktk masomo,Ukiona tabia zao sio nzuri ni vyema kurudi kwa "warden" akubadilishie chumba!
Naamini hayo hapo juu ndo ya msingi zaid japo yapo mengine mengi mtakayokutana nayo mkifika huko
MAZINGIRA YA CHUO
Chuo kwa ujumla ni kizuri na kikubwa,Naweza kusema kwa Tanzania hakuna wanafunzi wanaoishi vizuri na wenye mazingira mazuri ya kusoma chuon kama UDOM,madarasa ya kutosha,huduma mbalimbali kama maduka,benki n.k vinapatikana ndani ya chuo!Kila college inakila kitu chake inajitegemea "cafeteria,library","dispensary",hostel,maduka,ATM machines n.k!
Maji ya Dodoma sio mazuri kwani yana magadi hivyo maji ya kunywa inakubidi uwe unanunua ya kwenye madumu ya lita 5/10(Uhai) yanapatikana maduka ya chuo!Maji kwa ajili ya matumizi menngine kidogo yanasumbua kwa baadhi ya "colleges" hivyo ni muhimu kuwa na vyombo vya kutosha kuhifadhia maji pindi yanapokatika uwe una akiba chumban kwako!
Hayo ni baadhi tu ya mambo yaliyopo chuo,mengi utakutana nayo ukifika!
Kwa maelezo zaidi unaweza kunitafuta kwa namba 0753651270,0656759802