Indume Yene
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 2,962
- 721
Katika hali isiyotegemewa, Rais Jakaya Kikwete amekumbwa na kigugumizi cha utoaji vyeti kwa wale waliosaidia kuchangia ununuzi wa pikipiki kwa makada wa SISIEMU. Fisadi huyo ni Japhet Lema anayejulikana zaidi kwa jina la NJAKE.
Pikipiki hizo zenye thamani ya millioni 24.5 zilikuwa zigaiwe kwa Makatibu wa Chama wilayani Arusha. Mgeni wa heshima katika utoaji huo Rais Kikwete alichezwa na machale ya kuzigawa hizo pikipiki pamoja na vyeti baada ya kugundua kuwa Fisadi Njake ni mmoja wa wadhamini waliochangia ununuzi huo. Hivyo aliutupa huo mpira kwa viongozi wa chama hicho wilayani ili waweze kujigawia.
Hata hivyo danadana ilianza baada ya viongozi wa wilaya nao kuanza kurushiana mpira.
Hii inatia aibu sana, kwa nini Mwenyekiti wa SISIEMU(T) ambaye ni Rais wa JMT asiamuru kurudishwa kwa fedha alizotoa fisadi kununua hizo pikipiki badala ya kurushiana mpira? Bado hizo pikipiki zitatumiwa na SISIEMU, kwa hiyo JK kuruka viunzi na kuchomoa kugawa pikipiki kwa makada wake bado hakuleti unafuu wowote. Hizo ni baadhi ya pesa za wizi zilizonunua hizo pikipiki kwa ajili ya usafiri wa makada wa SISIEMU.