Fisadi wa Rada, Tanil Somaiya afanya kufuru IKULU


RAFIKI YA JK
Nataka kuchangia hiyo ya 5
ndo maana tunasema ccm itoke kabisa kwa sababu tunauchukia mchezo wa ccm na hatumchukii huyo rafiki yako.
kwa hiyo kama hoseah anakashfa za ufisadi asiseme ukweli amerepent na tunataka wanaccm mafisadi mtubu pia.
Hii ya kusema mbona hata flani yupo hivyo ni kufanya mapambano yawe magumu zaidi tunafanya kwa ajili ya nani sasa.??
 
Hili ndilo Ombwe la uongozi ambalo uongozi wa CHADEMA umekuwa ukijaribu kulinusuru Taifa kuondokana nalo. Taifa liko kwenye hangover kubwa ya uongozi, watanzania wenye mapenzi na nchi hii tuendelee bila kuchoka kuliombea Taifa letu na kuwaelimisha wenzetu wachache waliobaki na mawazo mgando kutoendelea kushabikia ujinga huu.

Dr. Slaa alisema wakati wa kampeni zake kuwa ni hatari na janga kubwa kuendelea kuliacha Taifa hili mikononi mwa huyu mkwere na CCM ulaji yake! CCM ya Nyerere haikuwa hii tunayoiona leo, na wala haitakuwa tena. Hiki ni chama kinachosubiri kifo chake mwaka 2015, maana wengi waliomo humo ni viongozi maslahi, kikipoteza madaraka wataikimbia hata nchi na ndio maana wanajilimbikizia mali wakijua kuwa wako mguu mmoja ndani, na mguu mmoja nje.

Mungu tusamehe watanzania kwa ujinga huu, endelea kulikumbuka Taifa ulilolipenda sana, tujalie nguvu ya kulirudisha Taifa lako mikononi mwa wazarendo kabla au ifikapo mwaka 2015.
 
Hao Ndio # wani bana... Wamesubiri uchaguzi uishe waongeze umeme na mgao kutuadhibu kwa kutunyenyekea miezi m3 ya kampeni!!
Na bado wnatulipisha deni la Dowans!!
 
Nahisi MUNKALI kunipanda baada ya kusoma post 64 zilizotangulia. Hili ni swala dogo kwa kimo lakini ni kubwa kimaudhui kutokana na mazingira yanahusiswa na huyo mtu na hizo preferential treatments. Kama hii taarifa ni ya kweli basi sina la kusema.
 
...Kishongo, hekima ya jibu inasema 'if you say that is not X then say it is Y' sasa tuambie ukweli ulivyo. Otherwise, karibu supu ya pweza hapa Tanga Resort Beach!
 
Duuuh, mimi nilikuwepo kwenye dhifa hii. Kwa kweli niliona kuna sports car kali nyekundu imepaki ndadi ya Ikulu tena nikajiuliza na mwenzangu ule mchuma wa Ridhiwani nini mbona umepaki ndani ya Ikulu wakati wote tumeambiwa tuache magari nje. Kumbe ilikuwa ni FERRARRI ya Tannil Somaiya? Toba!
 
Nachukia kuona Rais anakenuakenua meno kama mbayuwayu

Mhh...watu wana hasira. Nadhani lets us convince all eligible people to vote in 2015. I believe if only 70% of elligible people votes then mabadiliko ya kweli yatakuwepo.
 
Mbona tittle na habari haviendani? Nini maana ya kufuru? Au wewe hujui kiswahili? Kweli wewe ni zezeta.
 

Hadi mwaka 2015 tutakuwa tumechoka na hizi habari.
 
Kishongo ukitaka tukuamini lazima utuambie hao walinzi ulikutana nao lini? Na kwa shughuli gani? Na vile vile ulijuaje ya kuwa ni walinzi waliokuwa kwenye zamu siku husika?

Ili nini? Maana hapa siyo mahakamani kama hutaki kuamini kaa kimya endelea na mambo mengine! Vinginevyo kwa lugha nzuri ntasema Umetumwa wewe kawaambie waliokutuma kuwa umemkuta hayupo
 
tanzania ni nchi pekee duniani ambayo licha ya kutokuwa na kiongozi wa nchi (rais) wananchi wake wanaishi kwa amani.
 
hakuna hata mmoja aliye corroborate hii hadithi?

Nakubaliana na wewe, jee hakuna wengine waliokuwa hapo kwenye sherehe?

Hii story hata na mimi nina imani ni ya kutungwa labda kama kuna evidence ya picha.

Kwanza yeye kuruhusiwa kuingia na gari maafisa usalama pamoja na walinzi wa Ikulu walikuwa wapi? Halafu hapo tulipoelezwa amepark hiyo gari yake, ina maana hao maafisa wote walisinzia tu?
 
Hata wakati wa Mwinyi mambo yalikuwa similar na tunavyoona sasa.................... Nchi hii inawataka watu kama Slaa na Pombe Magufuri then heshima ya serikali itarudi.

Ongeza na Prof. Anna Tibaijuka.
 
Hata wakati wa Mwinyi mambo yalikuwa similar na tunavyoona sasa.................... Nchi hii inawataka watu kama Slaa na Pombe Magufuri then heshima ya serikali itarudi.



samahani magufuli ni wale wale hana moral authority kukemea uovu so my friend choose another one to compare with dr slaa and not magufuli!
 
Mkubwa hii ndio Tanzania yetu ya miaka 49 ya uhuru na hao ndio viongozi wetu ila wakumbuke "every begining has an end" na "What goes around comes around"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…