Fiston Abdoul Razak: Kheri nusu shari kuliko shari kamili. haikua bahati tu, bali ni neema ya siku ya jumapili ya tarehe 5 ya september 1993

Fiston Abdoul Razak: Kheri nusu shari kuliko shari kamili. haikua bahati tu, bali ni neema ya siku ya jumapili ya tarehe 5 ya september 1993

TEAM 666

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
4,399
Reaction score
8,594
KHERI NUSU SHARI KULIKO SHARI KAMILI . Haikua bahati tu , bali ni neema ya siku ya jumapili ya tarehe 5 ya September 1993 kwenye uzao wako mtukufu , haikua baraka ya jiji la Bujumbura tu , bali nchi nzima ya burundi ilinufaika na ujio wako duniani.

Nyota ilianza kung'aa mapema sana , tangu ulipopata mafunzo ya soka pale Lydia Ludic Burundi Academy , tangu hapo kila mrundi alijipiga kifua kwa kujua utalisaidia taifa hapo baadae.

Haikua ajizi kwako , kiwango chako kilikusafirisha nchi nyingi , Halitasahaulika goli lako moja kunako Mamelodi soundows ya Afrika kusini.

Ni nani asiye enzi mchango wako pale Luanda Angola knako Desportivo de agosto . Ipo haja ya kuvikwa kilemba cha uhodari kwa kazi uliyoifanya kule Al Zawraa nchini Iraq , kote ulitembeza soka safi.

Waarabu wa Misri na Algeria watabaki na jina lako tu , uliwafundisha jinsi ya kucheza kama striker wa kisasa . Naomba nikueleze tu , Wananchi wana imani kubwa na wewe , Hakuna anayetia doa rekodi zako ulizoweka barani Afrika , haikua rahisi kwako kufunga magoli 16 kwenye mechi 20 za timu ya taifa , ni nani aliyewaza kuwa utamzidi Mo salah kwa magoli kule Afcon .


Ni nani asiyejua ulikua sawa na ODIO IGHALO wa man U ?. Inatosha kuelezea ubora wako , karibu timu ya wananchi , wawekezaji pia ni wananchi , hawa ni watu wenye hamasa kubwa sana , wakitaka jambo lao liwe na linakua

. Karibu kwenye jangwa lenye neema na baraka , jangwa lisilo na njaa , jangwa safi.

sportsarena_tz-___CKElVGBAw3K___-.jpg


Wananchi wanataka uwape ladha ya Amisi Tambwe kwenye mchuzi wa Donald Ngoma, wape Tamu za Sunday Manara kwenye icecream yako.

Na ukifanya hivyo , jina lako litakua na utukufu mara mbili ya sasa.

Busara za ndugu yako Ntibazonkiza zikufikishe kwenye ukuu wa jina lako kwakua mnafahamiana na mtacheza soka safi .

Fiston naomba nikung'ate sikio tu , wananchi wanahitaji magoli , kama hutojaaliwa kuwapa vyote ulivyonavyo , basi wape kwa uchache na usiwanyime vyote.

Rekodi zako zimeingia kwenye vichwa vya wananchi , nenda kaziongeze kwa kugongelea misumari ya magoli Ni kheri uwape nusu ya furaha kuliko kuwanyima kabisa .

Chonde usije zifuta . Kila la kheri striker.
 
Mbona kila timu aliyosajiliwa amecheza mwaka mmoja mmoja, nini tatizo? Hata alikopelekwa kwa mkopo wakamuachia baada ya mwaka, na hakurudushwa timu iliyokopesha, akaenda nyingine.
 
Mbona kila timu aliyosajiliwa amecheza mwaka mmoja mmoja, nini tatizo? Hata alikopelekwa kwa mkopo wakamuachia baada ya mwaka, na hakurudushwa timu iliyokopesha, akaenda nyingine.
Maswali hayo na mengine yatajibiwa uwanjani.
 
Back
Top Bottom