Fitness and wellness

Uno more, cardio hip hop work out. Total body work out. Kwa wadada tu please. 🙂

Justin Bieber - Sorry | The Fitness Marshall | Ca…:
Yani hapa ndo mazoezi ntafanya sasa, bila music mmmmh
 
Reactions: kui
Mkuu inawezekana kabisa kupungua na kuishi healthy pasipo kwenda gym wala kutumia overpriced equipments. Nikupongeze kwa kujua na kuthubutu kuchukua hatua

Itakubidi mfumo wa maisha yako ubadilike ili kufikia malengo yako. Einstein alisema “The definition of insanity is doing the same thing over and over again, but expecting different results", hivyo inabidi ujiandae kubadilika, ukubali kubadilika ili uone mabadiliko.

Ili kupungua nashauri ufanye weightlifting na cardio kwa pamoja. Unaweza kuanza na push ups au nusu push ups kama huwezi kufanya push ups (yani weka magoti chini halafu fanyisha upper body huku magoti yakiwa chini hadi utapozoea na kuwa strong enough kufanya fully push ups). Cardio unaweza kuanza na jogging, running au kuruka kamba taratibu jioni au asubuhi.

Aidha ningeshauri utumie formula ya HIIT (High intensity interval training) katika cardio workouts mfano kama unakimbia 1km in 20mins jitahidi uweze kukimbia umbali huo huo for less than 20mins huku ukichukua breaks fupi fupi katikati, itakubidi u sprint hadi mwisho wako halafu pumzika Kidogo then kimbia tena.

Mazoezi si kitu kama eating habits zako hazitabadilika I can't stress this enough. Eat clean train dirty is the ruling formula in this world. Vyakula vya mafuta na sukari inabidi upunguze sana kama si kuacha kabisa bila kusahau pombe, chips na soda. Kula reals food and whole foods. Vyakula bora vyenye kujenga mwili ni kama sweet potatoes, brown bread, wali na mboga kama samaki, nyama, kuku, mayai, veggies,fruits nk. Kunywa Maji ya kutosha kila siku

Anza mabadiliko taratibu ukipunguza kimoja baada ya kingine, wanasema unaweza kuacha tabia yeyote kama utaenda mwezi mmoja bila kufanya hicho kitu so Jaribu kukaza hata mwezi bila kunywa soda uone kama baada ya hapo utaendelea kuwaza. Kwa kubadilisha ulaji wako utaona mabadiliko ukiongeza mazoezi utaona mabadiliko zaidi na kwa kasi.

Mazoezi kama kitu kingine chochote kwanza inabidi uamue na baadaye utazoea itakua sehemu ya maisha yako. Jitahidi hata kwa kujilazimisha Ufanye mazoezi kwa week at least siku 4 kwa muda wa miezi sita nakuhakikishia hutoacha tena. Mazoezi yanataka nidhamu na uvumilivu, kwa hakika hutobadilika overnight ila in time utaanza kuona mabadiliko, usikate tamaa kuwa mvumilivu. Good luck mkuu
 
Mkuu nimekuelewa na nashukuru kwa ushauri wako. Kesho nitanunua kamba. Viatu (raba na nguo za mazoezi ninazo). Nataka niulize natakiwa nifanye mara ngapi. Na unashauri nianze kwa muda gani. Hapa namaanisha discipline zaidi. Vile vile natakiwa niwe na ulaji wa namna gani naomba hata hits tu. Ujanipa daily intake ya food. Ili niweze kwenda sawa. My body type is endomorph. Na pia huwa nina tatizo moja. Ninapo fanya mazoezi day 1. Nikiamka day 2 mwili huuma sana. Watu wanasema inabidi ufanye tena. Ila maumivu ninayoyapata huwa nashindwa hiyo inasabanishwa na nini mkuu na kuna way ya ku prevent. Vile vile mkuu naomba nikushukuru kwa mchango wako. Ubarikiwe msinichoke



Cc : Nyani Ngabu
 

AgentX,

Hayo maumivu ni kawaida sana. Yanaitwa DOMS [Delayed Onset Muscle Soreness].

Huwa yanatokea pindi ufanyapo mazoezi au shughuli ingine yoyote ili ihusishayo misuli na shuruba.

Sababu huwa ni michaniko midogo midogo ya hiyo misuli kutokana na kuvutika na kutunishwa kuliko kawaida.

Kuyazuia kabisa hayo maumivu haiwezekani. Bali, unachoweza kufanya ni kuwa mwangalifu na intensity ya mazoezi hapo mwanzoni mwanzoni mpaka hapo mwili utapozoea hiyo hali mpya ya mazoezi.

Kwa kadri utavyozidi kufanya mazoezi ndivyo na misuli yako itavyoizoea hiyo hali na kupunguza ukali wa maumivu.

Ila kumbuka pia kuwa hata baada ya mwili kuzoea hiyo hali ya mazoezi, pindi utapoongeza intensity ya mazoezi, bado hayo maumivu utayapata ingawa yatakuwa si makali kivile.

Kwa hiyo hilo lisikutie hofu. Baada ya siku tatu au nne hivi utaona yanaanza kuisha tu yenyewe.

Jingine ambalo ningependa kukushauri ni kuyafanya mazoezi kuwa jambo la kufurahia.

Unaweza kufanikisha hilo kwa kufanya mambo kadhaa, machache yakiwemo kufanya mazoezi ukiwa katika hali ya usafi, kuyafanyia sehemu ambayo unapenda kwenda [kwa mfano mimi napenda kukimbia ufukweni mwa bahari au wa ziwa], kusikiliza muziki, na kuvaa vizuri.

Mimi huwa siwezi kwenda gym nikiwa sijaoga na kujiulizia manukato [body spray]. Hii hunifanya nijisikie niko msafi na niache kujistukia stukia kama ninawanukisha harufu mbaya wengine waliopo karibu nami. Nisipojistukia naweza ku focus zaidi kwenye mazoezi.

Pia naamini katika kuwa mtanashati hata nikiwa gym. Navaa viatu vizuri, suruali nzuri ya mazoezi, tisheti nzuri na safi, na kadhalika.

Nadhani kwa sasa hayo yanatosha. Baadaye tutafahamishana kuhusu proper form na anatomy.

Ni muhimu sana kuijua anatomy ili kuweza kujua aina ya mazoezi unayopaswa kufanywa kulingana na kiungo cha mwili.
 

Fanya mazoezi at least 4times a week muda wowote ule upatapo nafasi iwe asubuhi, mchana au jioni. Kama sasa una muda zaidi fanya hata sessions mbili kwa siku. Binafsi huwa session yangu moja ni saa1 ila nikiwa na nafasi nafanya zaidi na kama sina basi nafanya nusu saa ila najitahidi isiwe chini ya saa1. Nashauri ufanye weightlifting kabla ya cardio

Kuhusu food intake ni personal kwa kila mtu sababu miili yetu hurespond differently hili utazoea na kusoma mwili wako as time unfolds ila huhitaji kushinda njaa na since wewe ni endomorph unajenga muscles easily eating shouldn't be a problem to you. Kula shiba ila zingatia kula real and whole foods. Bodybuilding ina burn more calories hivyo kama hutokula vizuri mazoezi yatakula muscles badala ya fat.

Kula milo yote mitatu ya siku ya nguvu na snacks katikati kama utasikia njaa ila mlo wa usiku uwe at least 2hrs before bedtime. Unajua tatizo sio msosi tatizo ni ile energy tunayopata kwenye msosi inakaa mwilini bila kutumika, kama utafanya mazoezi vizuri esp weightlifting pushing yourself to the limit msosi wote mwilini utaisha so eating shouldn't be a problem at all. Personally nakula zaidi sasa kuliko zamani kabla sijaanza mazoezi na nimepungua ila nguvu zimeongezeka.

Maumivu baada ya mazoezi hilo kila mtu hu experience mwanzoni sababu mwili unakua haujazoea ila bdae huisha. You have to push through the pain mkuu Hakuna njia nyingine. Siku ya kwanza ukianza mazoezi ukiumwa kesho yake rudia tena maumivu yakipungua kabla hayajaisha kabisa do it repeatedly back-to-back kama week baada ya hapo yataisha kabisa.

Tupo hapa kusaidiana mkuu anytime tucheck tutashauriana na kusaidiana. That's the spirit Man. Good luck
 
That's my men. I am on the progress.
 
Mkuu hivi vitu ukivifuatilia unafanikiwa bana....nilikuwa kibonge wa kilo 89...nikajifua sasa Nina kilo 73 ....yaani natamani kuvua shat hata mbele ya watu waone sixparks zangu...tshrt na jeans sasa hakuna inayonikataaa...unene ni balaaa
 
Mkuu hivi vitu ukivifuatilia unafanikiwa bana....nilikuwa kibonge wa kilo 89...nikajifua sasa Nina kilo 73 ....yaani natamani kuvua shat hata mbele ya watu waone sixparks zangu...tshrt na jeans sasa hakuna inayonikataaa...unene ni balaaa
Tupe siri ya mafanikio yako. Umepoteza izo kilo 16. Kwa muda gani?
 
Tupe siri ya mafanikio yako. Umepoteza izo kilo 16. Kwa muda gani?
Miez sita....siri ya mafanikio ni ....niliacha kula vyakula vya mafuta na sukari kwa wingi....mfano niliacha kabisa kunywa soda....chakula changu hakikuzid ngumi yangu....nakula mboga za majani na matunda kwa wingi.....asubuh kabla ya kifungua kinywa nakunywa Maji ya uvugu ya tangawiz na limao.....mazoez jogging na ya viungo
 
Mkuu hivi vitu ukivifuatilia unafanikiwa bana....nilikuwa kibonge wa kilo 89...nikajifua sasa Nina kilo 73 ....yaani natamani kuvua shat hata mbele ya watu waone sixparks zangu...tshrt na jeans sasa hakuna inayonikataaa...unene ni balaaa
Kilo 89 ni kibonge?

Una urefu gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…