Fitness and wellness

Fitness and wellness

Wakuu Nyani Ngabu na Bufa salaam.



Niweze kukiri mwezi wa 5 nilipima BMI yangu nikaambiwa ni fat. Na natakiwa nianze mazoezi. Nikapuuza,kwangu swala la self motivation ni mtihani kwani sikuwahi kuwa mtu wa mazoezi. Toka mdogo mpaka ukubwa ni mnene. Na type ya body yangu ni endomorph na nikiri nina ulayi wa milo miwili lakini ni mbovu. Ulaji wangu unasikitisha. Mi pespsi na mi carbs kibao. Kwa mwili wangu sasa unakuwa na kitu kinachonikasirisha na kuja kuomba ushauri. Naanza kuona strech marks. Na sweat sana now days. Pia naanza kuona suruali zangu (namba38') zinaanza kunibana mapajani. Nikiri kwamba mpaka sasa toka mwaka uanze nimevaa namba 2. Yaani 36 alafu fasta 38 yaani nilinenepa. Fasta na suruali hazikunitosha ndani ya muda mfupi. Juu nava XL ila naanza kuona mikono ina tight sana na nyingine zinachanika.


Nimekuja hapa mnipe njia sahihi. In short huku nilipo mbagala... Hakuna gym za kisasa. Na mimi sio mtu wa mitaani sana wala pia sijui gym za mtaa. Ila kun sehemu napita kwenda kupanda daladala kuna uwanja wa polisi huwa watu wanakimbia kimbia. Kwa sasa niko free sina cha kufanya kwa miezi hii ilobaki mpaka vyuo vifunguliwe. Naomba unipe sheria na ushauri nifanyeje ili niwe na mwili wa avarage tu. Nataka niwe na kilo za kawaida. Mara ya mwisho kupima nilikuwa na urefu wa 5.8" na uzito wa 79. Sasa niambie nifanyeje. Umri ni Early 20s. Sasa nipeni somo wakuu hiki kitambi kipungue na hii minyonyo nachukia japo niko comfortable. Nataka niwe na mwili wa kawaida . nipeni darasa. Kutokaana na mazingira yangu yalivyo. Nakunywa bia pia .... And i smoke.


Nataka mwezi wa 10 nifanye shopping ya funga mwaka. Hofu yangu ni kuwa naweza kwenda kuvaa namba 40 kwa kipindi hicho. Kitu ambacho ni hatari sana. Naomba mnijuze wakuu.


Nini nifanye sina uelewa wowote wa mazoezi.



Nb; sina uwezo mkubwa wa kifedha
 
chips siyo ishu sana nitakuwa nakula mara moja kwa mwezi.
Mm napenda sana chips yaani nitafanya mazoez lakn chips nitakula hata mara moja lw wik mbili hiv au tatu
 
Mimi nina 175cm nina kg 76 natamani sana kupungua nifike 70 ila inashindikana, nakula mara moja kwa siku mchana na usiku nakula matunda au greens, sinywi bia huwa natumia pombe kali ila mara moja moja, inshort kwenye kula nina nidhamu, kukimbia nashindwa sababu nakosa company, mwili wangu ni mwepesi yaani sijaludhikana nyama wala sina tumbo mpaka sometimes nawaza labda ni u-giant maana baba yangu na mama wote ni warefu. Msaada tafadhali.
Kama vyote huwez basi jaribu kutafuta cd za mazoez ufanye muda wowotw ukijisikia huko chumban kwako
 
Fanya mazoezi yako kuwa rahisi,utaenjoy sana
Nni kweli kabisa,yaan utakuta mtu anafanya mazoez makali kisa kamuona fulan anafanya hvyo!mm naenjoy sana mazoez na huwa na shauri watu hayo niyafanyayo,nina cd zangu za aerobic kila siku nafanya lisaa limoja nikitok hapo nimesweat halafu nina raha maana unajihisi uko nao!
 
Mm nna kitambi cha bia
Naamuaga kufanya mazoezi kinaisha lkn kikiisha naacha mazoez kinarudi khaaa
Ss hv kimezidi
Mazoez nafanya leo kesho kutwa naacha cjui nifanyeje jaman khaa
 
Mm nna kitambi cha bia
Naamuaga kufanya mazoezi kinaisha lkn kikiisha naacha mazoez kinarudi khaaa
Ss hv kimezidi
Mazoez nafanya leo kesho kutwa naacha cjui nifanyeje jaman khaa

Yafanye mazoezi yawe sehemu ya maisha yako kama vile kuoga au kupiga mswaki.

Unaweza ukakaa siku mbili au tatu bila kuoga au kupiga mswaki?
 
Some useful pointers on how to stay motivated:

Tuanze na muziki.

Napenda sana muziki. Hivyo huwa najaribu kuutumia katika nyanja mbalimbali za maisha yangu ikiwemo kufanya mazoezi.

Siwezi kwenda gym bila iPod yangu. Kufanya mazoezi bila kusikiliza muziki sasa hivi siwezi.

Muziki hunifanya nilenge katika kukikamilisha kile nilichokipanga kwa sababu unaniondolea kelele zingine kama maongezi ya watu, vyuma kugongana, na kadhalika.

Kwa mfano nikiwa najiandaa kusukuma uzito mzito kwenye bench [bench press] ngoma ambayo naipenda na inayonipa mzuka ni Ruff Ryder's anthem ya DMX.



Nikiwa nataka kupiga 21s [bicep curls] napendelea kusikiliza We Right Here ya Dark Man X huyo huyo.



Aggressive style yake hunipa mzuka sana wa kuvishambulia vyuma.

Ninazo nyimbo zingine nyingi tu kwenye iPod ambazo huwa nazisikiliza nikiwa nafanya mazoezi.

Uzuri siku hizi kuna earphones zisizotumia miwaya kwa hiyo ni mwendo wa wireless tu. Napendelea zaidi za Beats by Dr. Dre

5565002_sd.jpg;maxHeight=550;maxWidth=642


Kwa hiyo kama mtu unatafuta kitu cha kukufanya uendelee kuwa motivated na kufurahia workout session yako jaribu kuushirikisha muziki uone matokeo yake.
 
Back
Top Bottom