Wakuu mimi nina tumbo la kitambi. Kuna kipindi nilinenepa na kufika kg 83 na nilikua na kitambi haswa. Mwili ule ulinipa shida sana ukizingatia kazi zangu ni za kukaa muda mwingi. Baada ya kuona hali sio poa nikaanza mazoezi taratibu ili nipungue. Ikumbukwe kuwa height yangu ni 5.7ft hivyo utaona ni kwa jinsi gani height na weigth vilikua haviendani....
Baaasi bwana nikakaza na mazoezi nikaoungua kidg hivyo yale maumivu ya mwili na uchovu wa mara kwa mara vikaniisha nikawa vizr na mazoezi nikaacha.
Lakini kuna kitu kimoja kizuri niliona, baada ya yale mazoezi mwili ulijengeka kdg hivyo nikivaa nguo hasa za juu zikawa zinapendeza sana.
Mwaka huu mwezi wa nne nikaanza tena mazoezi nikiwa na lengo la kutengeneza mwili sasa, nataka niwe na mwili mpana na ulijaa vyema ili nguo zikae vzr zaidi. Napenda mwili wa juu uwe kama ule wa *Rotimi. Huwa nakimbia mara tatu kwa week na nina uwezo wa kukimbia dakika 30 mpaka saa moja bila kupumzika. Nina eneo la mita kama 70 ndani ya nyumba ninayoishi ambalo lipo ndani ya uzio wa waya huwa nalitumia kwa ajili ya kukimbia. Kwa sasa nina pumzi ya kutosha. Kadhalika huwa napiga push up na kunyanyau uzito hapa hapa nyumbani na ninacheza mpira pia. Kwa kifupi mwili wangu umekua mwepesi na kwa sasa nina kg 74. Nina tairi pia kwa ajili ya mazoezi ya tumbo. Kwa sasa nafanya mazoezi ya uzito kuanzia jtatu mpka ijumaa. Jmos na jpili nakimbia, naruka, nacheza mpir nk.
Changamoto yangu ni kwamba mwili umechelewa sana kukata japo kwa sasa shape ya kifua inaonekana. Ninahitaji mwili mpana kuanzia tumbo mpaka kifua. Sitaki lile tumbo la kutokea kwa mbele.
Kitu ambacho naomba kuelekezwa ni kwamba nifanye nini ili niwe na mwili mkubwa bila kuwa na uzito mkubwa kupitiliza? Kiukweli sipendi kuwa na mwili mdogo na pia sipendi kuwa na uzito mkubwa sana ukizingatia kuwa sina kimo kirefu. Nataka niwe mwepesi kg zisipungue 70 au 75 ila umbo pana la mazoezi. Mtu ninaemwangalia kama kiigizo changu ni Rotimi, napenda niwe na mwili wa vile. Nitoe mfano wa mtu kama *Lukaku yule mwanasoka wa chelsea. Mimi sikuwahi kufikia ukubwa ule wa mwili lkn nilikua mzito sana sasa inakuaje yule jamaa katika umbo lile kubwa anakua mwepesi? Nawezaje kufanya mazoezi mengi na kuwa mwepesi na wakati huo huo nikaongeza mwili bila kuongeza uzito? Msaada wakulu.
Sent from my LG-D722 using
JamiiForums mobile app