Fiver na upwork

Fiver na upwork

Mo Issa

Member
Joined
Jul 28, 2020
Posts
43
Reaction score
93
Leo tujifunze kuhusu Fiver na Upwork.

Hello Habari wana JF

Ni imani yangu kuwa wote wazima na mnaendelea na majukumu ya kujenga taifa, na wale wenye changamoto mbalimbali zinazowakabili aidha kiafya, na hata kiuchumi namuomba Mungu wetu awafanyie wepes waweze ondokana na changamoto hizo.

Utangulizi
Kuna hiki kitu imani yangu watu wengi mmekuwa mkisikia au kujihusisha navyo (freelancing). Leo hii teknolojia imetufikisha mbali sana kiasi cha kwamba leo unaweza uza ujuzi ulionao katika majukwaa mbali mbali na kujipatia pesa itakayokidhi mahitaji yako. Nakupa mfano wewe ni mtaalamu wa lugha ya kiswahili na kingereza basi unaweza tumia ujuzi huo kujingizia pesa kwa kutumia majukwaa kadhaa ambayo leo tutaelezea mawili. Kwenye majukwaa hayo utaweza enda kufanya translation yaan kazi za kutafsiri lugha ya kingereza kuleta kwenye kiswahili na kiswahili kwenye kingereza. Mfano huo niliyokupa basi taaluma pia uliyonayo unaweza itumia kupata kazi za taaluma yako huko na ukaingiza pesa.

Hivyo basi kuna majukwaa kadhaa ambayo yapo yatakayokukutanisha wewe muuza ujuzi(freelancer) na wateja(clients) wenye kuhitaji hiyo taaluma yako... haya twende haraka kwenye hayo majukwaa...

Tuanze sasa>>>

World population ipo estimated kuwa 8 Billions according to ILO 2020 kuna 188M hawajui wapi wapate kazi, 120M wamekata tamaa kutafuta kazi na 165M wanafanya kazi wasio pendezwa nayo..almost Half Billion wapo frustrated na issue ya kazi (Source ilo.org/global/research..)

Akitokea mtu wakusolve unemployment rate atakua na value .

Leo tuone kampuni mbili Fiverr na Upwork, utakua umewahi kusikia au pia unajitengenezea kipato kupitia Fiverr.

Fiverr ni soko la kuuzia ujuzi (skills) ambapo inakutanisha kati ya wanye ujuzi (Freelancer) na clients.

Ikiwa una skill flani, either Logo design, Web design, writer, photographer au skill yoyote unaweza kuuza na ukalipwa kuanzia $5 na kuendelea

So, Fiverr inarahisisha skills outsourcing, maana yake wewe upo Tz ila mtu wa Canada au US anakuajiri kumfanyia kazi flani na anakulipa,

Currently tupo kwenye digital world na hii itakua favorable kwa makampuni kama Fiverr kuvutia content creators kuuza skills zao, lakini pia wanasuluhisha unemployment kwa wenye skills lakini hawana ajira.

Fiverr inawarahisishia Business owners kupata wafanya kazi na kwa njia rahisi, mfano HR ataweza kuangalia hivi vitu
  • Reviews za creator flani,
  • Pia ataweza negotiate price,
  • Ataweza compare content creators maana wapo wengi,
  • Ataweza connect na creator kwa haraka zaidi.

Fiverr kama kampuni wanapataje faida?

Faida wanapata kupitia Transactions na Fees kupitia services zao.

Wanakusanya almost 27% fee kwa kila transaction kuzidi competitor wake Upwork.

Covid-19 imewasaida sana kupata customers kutoka 2.5M hadi 3.8M kwa mwaka 2021.

Biashara yoyote lazima kuna ushindani, Kwenye stock market kabla ya kufanya investment kwenye kampuni flani lazima uangalie strength yake over competitor.

Competitor mkubwa wa Fiverr ni Upwork.

Upwork imetangulia kuanza kabla ya Fiverr lakini Upwork wapo focused na projects za makampuni makubwa, Fiverr mwenyewe anafocus na small business owners (Hii sio competitive advantage).

Upwork alikua first Runner, Fiverr alifatia akawa innovative kumzidi Upwork (CA), wanafaidika sana na business framework kupitia website yao. (fiverr.com/s2/29cbc4544a)

Namba ya customer ni kubwa kupita Upwork, so Fiverr wataendelea kuwavutia Business owners kwa siku nyingi zaidi.

Fiverr current price ipo around $205, market valuation ikiwa $7.3B. Highest price imefika $330

Good thing about Fiverr utaweza kunufaika kama owner wa kampuni kwa kununua hisa zake lakini pia unaweza kua Freelancer kwa kutengeneza contents na ukalipwa daily $5 above.

Baada ya miaka 10 naona Fiverr valuation yake itakua kubwa zaidi ya sasa hivi kwa sababu ya technology.

Lengo langu nikubadilisha wimbi la vijana kama mimi kwamba dunia inabadilika unaweza ingiza pesa kwa unachokielewa.

Nisamehe popote nilipoteleza
Ahsante kwa kusoma.
 
Asante sana mkuu. Najua vijana ambao wanapiga kazi uUpwork kwa muda sasa na hela ya kula na rent haiwapigi chenga. Kama ilivyo kawaida mwanzo ni mgumu maana inachukua muda kupata wateja na referrals nzuri lakini cha muhimu ni kuanza na kuaminika hasa kwenye ishu za deadlines na ubora wa kazi yako.
 
Uzi mzuri mkuu. Vijana wahamasike kufanya freelancing. Kulipwa kwa dollar, euro, gbp nk ni kitu kizuri sana

Binafsi nimebarikiwa kuweza kufanya mambo huko. Hasa ukipata kazi za hourly, hata kama ni $10, utasmile to the bank.

Mabahasha ya khaki yamehamia mtandaoni.
 
Kaka kama kweli umeajiri watu , put on a list siitaji kulipwaa .. ila tu nataman kuelewa hizi kazi maan nifanya graphics na video production
Kaka nashauri kama una ujuzi wa issue za graphics na video production majukwaa hayo yanakufaa na ni sehemu sahihi kwako ya kupigia pesa am telling you from expernce ndo maana nikaandika uzi huu utakuja hapa kunishkuru baadae. tumia ujuzi wako huo kufanya hilo.
 
Asante kwa uzi huu mzuri, nimeshatengeneza profiles huko Fiverr, Up work, na Freelancer, ila bado kuanza kuuza. Nitaanza kupost kazi kwenye akaunti yangu ya zamani ya LinkedIn ili kuvutia viewers kuja kuleta oda, ila Feverr ndo wanataka nitumie kompyuta Kuweka gig.
Bado sina kompyuta, ila nitaazima au kukodi ili niweke gig ya kwanza.
 
Ata simu inawezakana, weka simu yako kwenye "desktop mode" mi gig yangu ya kwanza Fiverr nilitumia simu Tena zile ndogo TECNO POP2 POWER
 
Asante sana
Asante sana Mtaalam, nimefaulu, nilikuwa nashindwa kubadili view kutoka mobile site kwenda desktop site [√] kwenye Google Chrome.
Nimetengeneza gig, na ndani ya robo saa nikaanza kupokea jumbe za watu wakitaka maelezo zaidi. Naamini nitasubiri kwa muda kupata order, ila gig ndo nishaweka kwa simu, nashukuru sana.
 
Attachments

  • 20230212062152.jpg
    20230212062152.jpg
    37.5 KB · Views: 65
Ata simu inawezakana, weka simu yako kwenye "desktop mode" mi gig yangu ya kwanza Fiverr nilitumia simu Tena zile ndogo TECNO POP2 POWER
Nimefanikisha, nina akaunti mbili, ili kuuza skills mbili tofauti (Electrical Engineering, kama ramani, Electronic Services kama logo design ).
Vípi nawezaje kujiuzia bila kula ban ili nipate reviews.
Pia hapo fiver nafanya test ili kuwa verified kwenye baadhi ya skills na experience, mfano, nimepata 6.2/10 katika Customer Care test, nimeongezewa kama verified skill.
Naomba usichoke kunielekeza namna nzuri ya ku improve kwenye hizi online jobs maana ndio soko la ajira la sasa na la kesho.
 
Back
Top Bottom