Fixed deposit kwa sasa hazina faida tena

Fixed deposit kwa sasa hazina faida tena

Habari wakuu

Leo nimeenda bank branch ya NMB nikawaomba wanifanyie hesabu ya milioni 40 kwa muda wa mwaka, wanadai hadi mwisho wa mwaka napata laki 240,000 kama faida

Sasa just imagine unawapa milioni 40 ndani ya kipindi cha mwaka mzima usubirie 240k si wizi huu!

Majizi Yapo Ndugu Zangu Hata Ndani Ya Ccm

Nasema Uongo Ndugu Zangu!!

Habari wakuu

Leo nimeenda bank branch ya NMB nikawaomba wanifanyie hesabu ya milioni 40 kwa muda wa mwaka, wanadai hadi mwisho wa mwaka napata laki 240,000 kama faida

Sasa just imagine unawapa milioni 40 ndani ya kipindi cha mwaka mzima usubirie 240k si wizi huu!
Waambie wao wakukopeshe iyo hela ili uone.
Banks Zina link wenye hela Ila hawana wazo la kuzofanyia na wenye wazo la kufanyia kazi hela sema hawana. Haina tofauti na Uber,Amazon wao Ni kuchukua Cha juu basi.
 
240k kwa 40m ni sawa na 0.6% ya pesa yote kitu ambacho haiwezekani. Itakua either hukuwaelewa au aliyekuelekeza amekuchanganya, hakuna rate ya hivyo bank. Wengi kama sio wote huanzia 5% - 7% kwa mwaka ambayo kwa mfano ikiwa 6% ya 40m itakua 2.4m kwa mwaka ( ambayo pia ni ndogo bado).
 
nikweli kabisa na nikamuuliza kwanini inakua hivi na ukiingia kwenye mobile yao unakupa data tofauti kabisa kwenye mobile app wanadai baada ya mwaka wanakupa milion 40% 2,160,000 baada ya kodi.

majibu aliyonipa baada ya kuhojii wanadai wanatoa riba kubwa iwapo wanataka pesa kwasasa pesa zipo.
Inawezekana kabisa aliyekupa maelekezo ni kilaza. Kwa Tanzania kwenda sehemu na ukapewa majibu yasiyo sahihi kabisa tena kwa jambo la maana sana siyo ajabu. Hata mimi bado siamini kuwa mil 40 kwa mwaka utapewa kiasi hicho.
 
Ahahaa, niliweka kakiasi fulani kwenye bank lakini baada ya kuchanganua kwa undani nikaona haya mambo yako overrated. Mwezi uliopita nikapitia pale kwenye tawi nikaawambia rudisha mpunga wangu nikafanye shughuli nyingne.

Nafikiri naweza kurudi endapo nitakua na uwezo wa kuweka walau kuanzia 1B.
 
SIO KWELI
SIO KWELI
SIO KWELI

Jaribu kusikiliza vizuri 240000 ni 0.6% ya mil 40. hakuna bank inaweka rate hiyo kwenye fixed deposit kwa mwaka.Nasisitiza HAKUNA
mkuu nakuomba uende nmb amini usiamini nilichokiandika ndicho walichoniambia na siamini kama bank watakua na muhudumu kilaza ashindwe kufanya hesabu wakati system anayo
 
240k kwa 40m ni sawa na 0.6% ya pesa yote kitu ambacho haiwezekani. Itakua either hukuwaelewa au aliyekuelekeza amekuchanganya, hakuna rate ya hivyo bank. Wengi kama sio wote huanzia 5% - 7% kwa mwaka ambayo kwa mfano ikiwa 6% ya 40m itakua 2.4m kwa mwaka ( ambayo pia ni ndogo bado).
jaribu kwenda tawi la nmb ukasibitishee
 
Sikia acha ujinga huo unahela nyingi ingia inbox nikupange ukafanye kilimo muwa wa sukari utanikumbuka usidhani tuliopo hapa mjini tunakunywa bia ukadhani ni wafanyakazi wa bandari wanaokopa mikopo wananywea bia na kutambishiana

Tena nitakushauri uaze na heka tano tu njoo nbox nikupange
 
tena ukiwauliza wanadai wanatoa 6% kwa mwaka sasa kama hiyo intrest ukipiga hesabu mbona sio 240k ni milion 2,160,000 baada ya Vat
Uwa hakuna makato ya VAT kwenye interest inayopatikana. Makato uwa ni withholding tax ambayo uwa ni 10% ya faida iliyopo.
 
Fixed deposit sio biashara ile mzee ...fixed deposit ni kwa ajili ya mtu mwenye pesa ambaye kwa wakati huo hana mipango nazo au kazi nazo hivyo anaenda kuziweka bank ili mtu ambaye kwa wakat huo ana mipango ila hana hela aje kuzikopa ili atimize mipango yake .ingekuwa fixed deposit ni biashara watu wasinge rake risk ya kufanya biashara
 
Habari wakuu

Leo nimeenda bank branch ya NMB nikawaomba wanifanyie hesabu ya milioni 40 kwa muda wa mwaka, wanadai hadi mwisho wa mwaka napata laki 240,000 kama faida

Sasa just imagine unawapa milioni 40 ndani ya kipindi cha mwaka mzima usubirie 240k si wizi huu!
Hivi hamna faida kbs
 
Japo bank ni wanyonyaji ila nahisi umechanganya madesa.

Milioni 40 kweli wakupe faida laki 2 na 40 kweli

Nahisi kuna sifuri umeisahau, ni milioni 2 na laki 4 ndiyo walipaswa wakupe.

Japo nayo ni ndogo sana kwa milion 40
Hata hivyo bado ni ndogo
 
Habari wakuu

Leo nimeenda bank branch ya NMB nikawaomba wanifanyie hesabu ya milioni 40 kwa muda wa mwaka, wanadai hadi mwisho wa mwaka napata laki 240,000 kama faida

Sasa just imagine unawapa milioni 40 ndani ya kipindi cha mwaka mzima usubirie 240k si wizi huu!
Kwani hujui malengo ya haya Mavitu
[emoji1485]Benki
[emoji1485]NSSF/PSSSF
[emoji1485]BIMA za MAGARI/MOTO/KIFO

Ukijua Malengo makubwa Basi Hutopeleka Pesa zako huko Ingawa System itakulazimisha
 
Back
Top Bottom