Nyuki Mdogo
JF-Expert Member
- Oct 31, 2021
- 4,134
- 10,644
Hio 240,000 una uwezo wa kuiingiza kwa wiki 2 kwa mtaji wa milioni 1.Habari wakuu
Leo nimeenda bank branch ya NMB nikawaomba wanifanyie hesabu ya milioni 40 kwa muda wa mwaka, wanadai hadi mwisho wa mwaka napata laki 240,000 kama faida
Sasa just imagine unawapa milioni 40 ndani ya kipindi cha mwaka mzima usubirie 240k si wizi huu!
nakwambia biashara ambayo naifanya wala sio kwamba mm ni motivational speaker😅😅
Anzisha biashara isiyo rasmi ya kukopesha wadau hapo mtaani
mkopo wa laki 1, riba yake ni 20,000 kwa wiki 2 (kwangu nabana kwa wiki 1 tu, this means kwa mwezi ni 80% kama mteja akiendelea kukopa pesa hio hio, sharti ni kuleta riba na kuendelea na mkopo}
Hakikisha unachukua vitu bondi vyenye thamani kubwa mara 2 ya mkopo uliochukuliwa. UWE SERIOUS SANA KATIKA SUALA LA BONDI NA UWEKE MAANDISHI. THIBITISHA KABISA MALI NI YAKE KABLA YA YOTE.
KUWA MAKINI MATAPELI NI WENGI SANA HAPA, WANAKUJA KWA LUGHA LAINI SANA WAKISHAPATA HELA WANAKIMBIA
kwa mtaji wa milioni 1 tu kwa mfano, kwa interval ya wiki 2, kwa riba ya 20%, unaingiza 400,000 faida.
TAHADHARI TENA;
Kuna watu si waaminifu, wanaweka bondi mali zisizo zao.
Kwa bondi kubwa zenye hati kama nyumba, kiwanja, pikipiki ama gari, jitahidi ukaandikishane kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa.
Hapa kwenye maandishi weka pesa jumla na mkopo wake. Usiandike kama umemkopesha isije ikakuletea shida baadae.
Aliechukua pesa aji commit kwamba endapo pesa haitorudishwa kwa muda mliokubaliana basi bondi yake iuzwe kurudisha fedha alizochukua kwako.
anza pole pole tu utakuja kuniambia utam wa hii biashara.