Flashback 2011: Alichosema Mhe. Kikwete Kuhusu Wanafunzi Kufeli (Miaka 2 iliopita)

mambomengi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2009
Posts
829
Reaction score
242


Akizungumzia kiwango cha ufaulu, rais Kikwete aliwataka walimu wanaotunga mitihani ya shule za msingi, sekondari na vyuo, kuacha kutunga migumu kupita kiasi, kwa kuwa yawezekana kuwa ndicho chanzo cha matatizo.

"Changamoto ya ufaulu mdogo kama mnavyodai katika masomo ya sayansi, hisabati na kiingereza pengine inatokana na ugumu wa mitihani... lakini msitunge rahisi sana," alisema na kuongeza ni lazima wahitimu wawe na viwango vinavyostahili.

chanzo : UhuruPublications, (via Source: wavuti.com (17/03/11))

Hali halisi kama alivyoripoti Kitila Mkumbo kwenye chati hii chini inaonesha kiwango cha kufaulu kipo kwenye mporomoko wa"freefall"--bila kufunga breki, "extrapolation" yangu inaonesha chini ya asilimia 2.5% watafaulu ifikapo 2015!
 
Si dhani kama mitihani inayotungwa leo hii ni migumu kulinganisha na miaka 10 au ishirini iliyopita. Ni vyema kungalia matatizo ya elimu yetu kitaalam zaidi kuliko majibu ya jumla jumla. Kuna waliamu, wenye moyo na ari ya kufundishwa, maslahi yao yakoje? vitendea kazi je? tuacha majibu ya kisiasa kuwa tumejenga shule mia au milioni nakuona kuwa nimeafanikio. Mafanikio tunahitaji kuyaona kwenye ufaulu wa watoto. Hii ni vita ndugu zanguni na ni lazima ipiganwe.
 
Tujiulize kwa nini ufaulu mwaka 2012 ulikuwa asilimia 77 na leo ni 34. Why, mitihani ilikuwa mirahisi? au kuna kitu tumevuruga na ni kwa makusudi ndiyo maana hatutaki kuliangalia hili tatizo kwa ukweli wake. Bahati mbaya sina takwimu hapa za jinsi ambavyo bajeti ya Wizara ya elimu inavyoongezeka mwaka hadi mwaka na maokeo yake badala ya elimu kuimarika inazidi kuporomoka.
 
Hayo ndo mawazo ya mtu dhaifu. Idd amin alipoambiwa kwamba uchumi unashuka, aliagiza zitengenezwe hela nyingi. Ndo haya jk,yeye si mtaalam wa elimu atajuaje kuwa mitihani inatungwa migumu
 
Mnapodadavua data na kuangalia miaka mitano ya nyuma ni kujifunga katika mahitimisho. Kiwango cha elimu kimeanza kushuka toka nchi ilipopata uhuru. Utandawazi ndiyo kwa sasa unatufanya tuweze hata kuwa na graphic picture kama hii, kwa msaada wa maelezo zaidi, jaribu kuangalia toka tupate ukoloni kwa plan ya muda mrefu na utambuzi mzuri wa tatizo/matatizo.

Ni kweli kama hakuna kitakachofanyika, kuna uwezekano wa ufaulu kuwa zero kwa vile hata zile shule za wenye 'vipaji' nazo ziko kwenye mporomoko pia.

Wanasiasa wetu wengi ni wazembe katika kauli zao (prone to gaffe) na haishangazi hata pale Rais anaposema maneno kama haya bila kufikiri tafsiri yake kwa jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…