mambomengi
JF-Expert Member
- May 16, 2009
- 829
- 242
Akizungumzia kiwango cha ufaulu, rais Kikwete aliwataka walimu wanaotunga mitihani ya shule za msingi, sekondari na vyuo, kuacha kutunga migumu kupita kiasi, kwa kuwa yawezekana kuwa ndicho chanzo cha matatizo.
"Changamoto ya ufaulu mdogo kama mnavyodai katika masomo ya sayansi, hisabati na kiingereza pengine inatokana na ugumu wa mitihani... lakini msitunge rahisi sana," alisema na kuongeza ni lazima wahitimu wawe na viwango vinavyostahili.
chanzo : UhuruPublications, (via Source: wavuti.com (17/03/11))
Hali halisi kama alivyoripoti Kitila Mkumbo kwenye chati hii chini inaonesha kiwango cha kufaulu kipo kwenye mporomoko wa"freefall"--bila kufunga breki, "extrapolation" yangu inaonesha chini ya asilimia 2.5% watafaulu ifikapo 2015!