DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Massay alihama CCM wakati wa mchakato wa uteuzi wa wabunge, ambapo jina lake halikurudi katika hatua za awali. Siku chache baadaye alichukua fomu kugombea ubunge kupitia ACT-Wazalendo.
====================
FLATEI ATIMKA ACT, AREJEA CCM KUSAKA KURA ZA USHINDI
ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Mbulu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Flatei Maasai ametangaza kurejea CCM akitokea ACT Wazalendo ambako aliteuliwa kugombea ubunge kupitia chama hicho huku akisisitiza kumuombea kura mgombea Urais wa CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Akizungumza wilayani Mbulu akiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, Flatei alisema baada ya kuhama CCM alikutana na wazee ambao walimlea tangu akiwa mdogo wakimtaka kurejea ndani ya Chama.
"Inabidi uwasikilize wazee wanasema nini, na mimi ninavyojua wazee hao ni wazee wangu na kwa sababu hawa wazee ni wa Chama wamekuja kwangu, zaidi ni kuwasikiliza wazee hawa ili kuendelea kujenga Chama," alieleza.
Kwa upande wake, Wasira, alitoa wito kwa wanachama wa CCM ambao hawajateuliwa kugombea ubunge, kuendelea kumuombea kura mgombea Urais wa CCM Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa chama hicho.
Alisema kutoteuliwa kugombea nafasi hiyo siyo mwisho wa uanachama wa CCM kwani chama hicho kingeshakuwa kimepoteza idadi kubwa ya wanachama ambao hawajateuliwa kuwania nafasi hiyo kupitia CC.
"Mbona wapo wengine wanachama lakini siyo wabunge, lakini kazi za kujenga chama na kujenga nchi siyo Bunge peke yake, zipo nyingi hata kusimama kwenye jukwaa na kuwaambia chagua Samia. Hiyo ni kazi ya CCM ambayo huyu anaiweza na tumemwambia aende jukwaani akaombe kura," alisisitiza.
Soma Pia:
-
GE2025 - Flatei Massay awekewa pingamizi Ubunge Mbulu
Baadhi ya wanachama wa Chama cha ACT-Wazalendo katika Jimbo la Mbulu-Vijijini, Wilaya ya Mbulu, Mkoani Manyara, wamepeleka pingamizi la kumpinga Mgombea wa kiti cha ubunge kwa tiketi ya chama hicho Flatei Gregory kwenye ofisi ya msimamuzi wa uchaguzi jimbo la Mbulu vijijini kwa madai ya kuwa...
www.jamiiforums.com
-
GE2025 - Aliyekuwa Mbunge wa Mbulu Vijijini achukua fomu ya ubunge kupitia ACT Wazalendo baada ya kutopitishwa na CCM
Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mbulu Vijijini Flatei Gregory Massay amechukua fomu ya kugombea Ubunge katika Jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo. Amekabidhiwa fomu hiyo na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mbulu Vijijini Ndugu Joseph Sambo.
www.jamiiforums.com