Flaviana Matata azua utata wa uchumba

Flaviana Matata azua utata wa uchumba

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,222
Reaction score
4,689
MISS Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata amezua utata wa aina yake baada ya picha zinazomuonesha katika tukio la kuchumbiwa kunaswa na mwenyewe kudai si yeye aliyechumbiwa.

attachment.php

Miss Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata.



Kwa mujibu wa chanzo, tukio hilo limedaiwa kufanyika kwa siri hivi karibuni nyumbani kwa miss huyo, Shinyanga na kuhudhuriwa na baadhi ya ndugu wa karibu.

“Inaonesha hawakutaka watu wajue maana hata hakukuwa na watu wengi siku hiyo, hata hao ndugu wenyewe hawakuwa wengi kiivyo lakini picha zinaonesha Flaviana akichumbiwa,” kilisema chanzo hicho.

Kikizidi kumwaga data chanzo hicho kilidai kwamba, mwanaume anayetaka kumuoa mrembo huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja ni Mchaga mwenye fedha zake aishiye Marekani.

“Nasikia huyo bwana wake ni Mchaga lakini anaishi Marekani, atakuwa ana fedha zake si mtu wa hivihivi,” kilisema chanzo.

attachment.php


Flaviana Matata akiwasalimia wazee kwa kupiga magoti.


Amani lilifanikiwa kuzinasa picha hizo ambazo zinamuonesha mrembo huyo akiwa amepiga magoti huku amemshika mkono mmoja wa wazazi wake aliyeshiriki katika hafla hiyo ya kupokea mahari.

Baada ya kupata madai hayo, paparazi wetu alimtafuta Flaviana kwa njia ya simu ya mkononi ndipo alipokataa katakata kuwa si yeye aliyekuwa akichumbiwa bali ni dada yake.

“Hamna kitu kama hicho, unayesema alikuwa anachumbiwa si mimi ni dada yangu, mila za kwetu Shinyanga nalazimika mimi kumsindikiza hivyo kama umeona picha hizo uelewe hivyo,” alisema Flaviana.

Hata hivyo, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa ni la Flaviana na si dada yake hivyo kuzidi kuzua utata juu ya ukweli halisi, Amani linaendelea kufatilia kwa karibu.
 

Attachments

  • Matata1.jpg
    Matata1.jpg
    34.3 KB · Views: 2,348
  • Matata.jpg
    Matata.jpg
    19.6 KB · Views: 2,330
Kama kweli ni yeye kutakuwa hakuna penzi la dhati hapo,Atakuwa hayuko comfortable na mchumba wake.
 
Atakuwa mtu wa fedha zake, si wa hivihivi
 
Mzee A.Y vipi tena? ule ukaribu nilidhani future wife bana......
 
So what's the big deal hapa?

Au ndo Umarekani zaidi, celebrity akijamba shurti headlines, watu watafute chupa kumkimbilia wakinge ushuzi na kuuuza kama manukato?
 
mie aah, labda intokee tu....:A S wink:
 
Back
Top Bottom