Ninaona wewe unajua mambo mengi sana. Unaweza kutusaidia sana hapa kumaliza huu mjadala na wote tukaridhika kabisa kwamba pasipo shaka mtoto wa Flora si wa Emmanuel, na kwamba ni hakika ni wa mchungaji Gwajima.
1. Unaweza kukumbuka ni siku gani hasa ambayo Flora na Emannuel kwa mara ya mwisho walifanya tendo la ndoa pamoja? Hii itatupa mwanga wa kuondoa kabisa uwezekano wa Emannuel kuwa amezaa na Flora huyu mtoto.
2. Hiyo siku walipofanya tendo la ndoa mara ya Mwisho Flora na Ema, ilikuwa ni kipindi gani katika mzunguko wa hedhi wa Flora? Hapa utakuwa pia unatuongoza kujua kwamba kwa siku ile hapana uwezekano wa Flora kpata mimba hata kama itakuwa ni ndani ya miezi sahihi.
3. Ninaomba pia, kwa kuwa wewe ulina ushahidi kamili, hebu tuambia ratiba ya tendo la zinaa kati ya Flora na Gwajima ilivyokuwa pia ili tulinganishe na ile ratiba ya Emma.
4. Tunaomba utuambie vipimo vya DNA ulivyofanya kwa yule mtot vinasema nini.
5. Unaushahidi gani kwamba maneno yote anayoyasema Emanuel ambaye amethibitika kukimbilia kwenye media zaidi na kukosa uadiifu wa kifamilia kwamba ni ya kweli mpaka umpe haki 100%?
6. Kutetereka kwa ndoa, kutengana kwao, kutuhumiana kukombwa vitu, kutengana n.k, n.k, kulikosikika wakati Flora tayari ni mzamzito, kunaondoaje uwezekano wa kuwa mtoto aliyezaliwa na Flora ni wa Emma?
7. Tabia ya Emma kubaka mtoto wa ndani ya nyumba kwako ni halali tu na haina shida?
8. Unasemaje juu ya Emmanuel Mbasha kushindwa kukana tuhuma za kulala na mtoto wa ndani ambapo wewe unaashdadia kana kwamba unahakika emma ambaye hajakanusha hili, kwamba anasingiziwa?
Tafadhali acheni tabia za namna hii, haziwasaidii.
Emmanuel atakataaje wakati hakai pamoja na Frola, na hata hajamuona huyo mtoto? Halafu kwa nini kwa akili yako ya kawaida unategemea Frola akili kuwa ni mtoto wa Gwajima, kwani yeye Frola hajui aibu itakayompata? Na huyo Gwajima kwani hajui impact itakayotoea kwa waumini wake pindi akikiri kuwa huyo ni mwanae?
Labda nikurudishe nyuma, maana yawezekana umekurupukia tu hii mada na hujui imeanzia wapi na ni kwa nini watu wapo attention sana na suala la Frola kujifungua mtoto. Hebu pitia hizi mada chini kwanza