Ukichunguza maandiko mengi yanazungumzia ndoa kama kitu kisicho na ukomo hadi kifo.........sehemu ambayo baadhi ya Wakristo wanatumia kusimamia ruhusa ya talaka ni huo mstari tu ambao tafsiri yake bado inaubishani wa muda mrefu sana......lakini ukisoma Marko 10 katika mistari niliyoweka hapo chini utaona jinsi Yesu anavyosema juu ya Talaka .........baada ya ndoa mnakuwa mwili mmoja......neno mwili mmoja linafunga kabisa uwezekano wowote wa kuwepo watu wawili kutoka katika mwili mmoja ..........kila mstari utakaousoma hapa chini ni kamilifu na hautoi fursa ya kuvunja ndoa ...........suala ya utengano kiroho umeliandika kana kwamba utengano huo ukitokea basi unakuwa permanent......lakini tunaona hata tunapotenda dhambi tunakuwa na utengano na Mungu kiroho pia lakini kupitia kitubio tunaunganishwa nae ..............hebu tafakari vizuri maandiko haya mkuu .............
Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamwuliza, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe? Huku wakimjaribu.
3 Naye akajibu, akawaambia, Musa aliwaamuru nini?
4 Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha.
5 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii.
6 Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.
7 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
8 na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
9 Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
10 Hata nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza habari ya neno hilo.
11 Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake;
12 na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini.
Asante sana kwa hilo andiko Mkuu MTAZAMO. Kati ya maswala yenye mkanganyiko mkubwa ni swala hili.
Tukianza na uchambuzi wa huyu ndugu hapo niliko bold inabidi tena tukayachunguze maandiko kwamba ndoa inaanzia wapi? kuishi pamoja au inaanzia kanisani au inaanzia mtu yeyote mke na mtu mume wanapokutana? au watu wawili wanapokubaliana, na je tunaposema wanakuwa mwili mmoja, ni kimwili au kiroho? Na je? Mmoja wapo anapoenda kulala na mwanaume au mwanamke mwingine, kimwili na kiroho kunatokea nini? na hayo yanayotokea yaweza kutengenezwa au kurekebishwa na nini? n.k n.k..... Tukishafahamu muunganiko uliko wa mtu mume na mtu mke, ndio twaweza anza kujua kuvunjika kwa huo muunganiko kunatokea wapi na kwa weza sababishwa na nini.
Mfano katika kiapo cha ndoa makanisani kuna sehemu wanasema ... nitakua WAKO na Nitakuwa mwaminifu kwako hadi kifo kitakapo tutenganisha.....(Je kutokuwa mwamininifu madhara yake ni nini? Ni kifo au kupoteza nafasi au uhalali wake kama mke au mume?...
Kwa maana tunamuona Adamu akiambiwa na Mungu akila tunda alilokatazwa HAKIKA ATAKUFA... lakini hatuoni akifa kimwili bali tunaona akifa kiroho (positionally) kwanza kutoka chini ya Mungu hadi kuwa chini ya shetani.. then vingine vikafuatia kufukuzwa na kadhalika) sijui kama nitaelewka vizuri hapa.. mniwie radhi (Adam ndio alikua anatawala dunia lakini baada ya dhambi tunaona maandiko yakimsema Shetani kama Mtawala(controller) wa dunia, Mungu wa dunia hii, Mkuu wa ulimwengu n.k nafasi ambayo ilikua kwa Adamu .... uzuri ni kwamba baada ya Yesu kuja, Adamu wa pili hawi tena chini ya Mungu bali anatawala pamoja na Mungu.
Kwa hio mtu mume anavyotoka nje ya agano/patano kufanya uasherati, anapoteza uhalali au nafasi yake kiroho kama mume au mke. hatukioni japo tunawaona wakiishi ila spiritually they are disjoined/dis connected.
Unasemaje hapo mkuu? nini maoni yako!! Naona mjadala unazidi kuwa mgumu aisee!!! ukisoma hilo andiko Yesu alilokua akiwajibu wale majamaa kuhusu talaka unaona nini?
Many thanks