Biblia inasisitiza sana kusameheana na inasema asiye samehe wengine bila kujali aina ya kosa, basi hata yeye Mungu hatamsamehe mtu huyo.
Kuhusu kisa cha hawa wawili, Flora ndiye aliye mwacha Emma, wakati ule Emma alimbembeleza sana Flora wasahau tofauti zao warudi waishi kwenye ndoa yao lakini Flora alikataaa kata kata hata kumtia aibu mumewe. Wakati huo Flora alikuwa anahatia mbele za Mungu kwa kuvunja ndoa na kukataa msamaha wa mumewe.
maana biblia inasema mtu akikosa hata saba
mara sabini kwa siku akija na kuomba msamaha, msamehe.
Baada ya kesi kwisha, Flora alimtaka mume wake amsamehe warudiane, kakini Emma alikataa katakata. Hivyo hatia ikageuka kwa Emma.
Kwa sababu hiyo Flora amehesabiwa haki kwa sababu aliomba msamaha kabla Emma hajaoa lakini Emma alikataa, kibiblia hata Mungu hajamsamehe Emma dhambi zake kwa kukataa kumsamehe Flora. hivyo Emma anahesabiwa kama mdhambi tu aliye amua kumwacha mkewe.
Hivyo Flora aliye tubu anapata uhalali wa kuolewa kwa neno linalosema:- yeye asiye amini akitaka kuondoka na aondoke, ndipo huyo ndugu mume au mke yu huru.
Kwa sasa Flora yuko huru
kuolewa kwa sababu Emma kamwacha kwa kukataa kumsamehe pale Flora alipoomba Emma amsamehe warudiane.
Emma atabaki na hatia.
Biblia inasema heri kuoa au kuolewa kuliko kuwaka tamaa. Flora bado kijana sana. Hana hatia kabisa mwacheni aolewe amtumikie Mungu vizuri.
HAPPY WEDDING FLORA.