Mapengo 17
R I P
- Mar 28, 2014
- 1,229
- 610
SIKU chache baada ya minon'gono kuibuka chini chini kuwa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Tanzania ambaye pia ni Mke wa Emmanuel Mbasha, kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na Mchungaji wa Kanisa la kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima ameibuka na kukanusha madai hayo.
Akijibu maswali ya mashabiki wake wakati akichati moja kwa moja 'live' kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa Sita kamili amesema kuwa hawezi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu ambaye ni ndugu yake hivyo Mchungaji Gwajima ni mjomba wake na si mpenzi wake kama ambavyo watu wamekuwa wakizungumzia suala hilo kwa kile alichodai ni baadhi ya watu wanaotaka kumchafulia jina na hadhi aliyo nayo.
kumshushia hadhi."Hayo ni maneno tu ya watu mtaani ila Mchungaji.
Gwajima ni mtumishi wa Mungu na ni uncle wangu ninawezaje kuwa na mahusiano na uncle wangu..? "Alihoji Flora.
Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, Florah Mbasha, akichat Live leo katika ukurasa wa Facebook wa EATV.
Akijibu maswali ya mashabiki wake ambao wengi wao wakimtaka aeleze ukweli juu ya ugomvi uliopo kati yake na Mumewe au ni skendo tu za magazeti, ambapo aliweka wazi kuwa kuna vyombo vya habari ambavyo vimekuwa na lengo la kumchafua na kumualibia sifa ndio maana walitumia gharama kubwa kufanya wanavyoweza ili kutimiza malengo yao,mbasha amedai kuwa alimua kukaa kimya kwa kuwa hakukuwa na ukweli wowote.
"Hizo stori mnazosikia hazina ukweli wowote na ndio maana niliamua kukaa kimya sikutaka kujibizana kwenye vyombo vya habari kwa uongo wa baadhi ya magazeti ya udaku ila ninasikitika sana kwani kuna watu wamekaa na kujipanga kisawa sawa kwa ajili ya kuhakikisha wanaharibu huduma yangu kwa gharama zozote, lakini bado ninasonga mbele kwani mwanzilishi wa huduma yangu ni Mungu na huyo ndiye atakayeimaliza na sio mwanadamu. hata hivyo ninawashukuru kwa kuwa wamenitabilia nkuja kumiliki jumba na magari ya kifahari ingawa yote ni ubatili"
Adai hajaachana na Mbasha
Flora Mbasha amesema kuwa watu wengi wanasema kuwa ameachana na Mumewe kisa Gwajima hilo swala halina ukweli wowote hajaachana na Mbasha sababu ya Gwajima na amedai kuwa bado anampenda sana ila anampenda Mungu zaidi.
bali amekuwa na matatizo katika ndoa yake kati yake na mumewe na ni matatizo yao ya ndani ambayo asingependa kuyaweka wazi katika vyombo vya habari maana kufanya hivyo ni sawa na kumvunjia heshima mumewe,maana mambo ya chumbani ni siri yao wenyewe asingependa kuwa wazi sababu wanamtoto mkubwa sasa.
"Sijamwacha mume wangu sababu ya Gwajima na kweli bado napenda sana Mbasha lakini nampenda zaidi Mungu"
Wakati anazungumzia suala hili Flora ameweka wazi kuwa kwa sasa ni mjamzito na ujauzito huo ni wa Mume wake ambaye ni Emmanuel Mbasha, maana ameishi naye katika ndoa zaidi ya miaka kumi na katika kipindi chote hicho hajawahi hata siku moja kumsaliti Mumewe.