Florian Kaijage apigwa chini TFF

Muadilifu

Senior Member
Joined
Sep 26, 2007
Posts
149
Reaction score
23
Shirikisho La Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemsimamisha kazi afisa habari wake, Florian Kaijage (pichani) kutokana na fedheha ya kushindwa kutimiza itifaki muhimu ya kupiga nyimbo za taifa wakati wa mechi ya Taifa Stars na Morocco jumamosi jijini.

Rais wa TFF, Leodegar Tenga amewaambia waandishi wa habari jijini leo kuwa tukio hilo ni la aibu mbele ya Rais Jakaya Kikwete, mashabiki na wageni wengine na mbaya zaidi kwa vile mchezo huo ulionyeshwa katika luninga ndani na nje ya nchi, hivyo aibu hiyo imeshuhudiwa na wapenzi wa soka kote duniani.

Amesema TFF imemua kumwajibisha Kaijage kwa kuwa ndiye aliyekuwa amepewa jukumu la kusimamia jambo hilo. Aidha alisema wakati amesimamishwa kaijage ataisaidia timu itakayoundwa kuchunguza jambo hilo na kuongeza kuwa hatua zitachukuliwa kwa yeyote Yule atakayebainika kuhusika kwa tukio hilo.

Amesema jambo hilo halikustahili kutokea kwa kuwa liliishawahi kutokea wakati wa mchezo na Brazil ambapo safari hii wahusika walipewa jukumu la kuhakikisha kuwa wanazijaribu nyimbo zote siku mbili kabla ya mchezo na kuhakikisha kuwa hakuna hitilafu yoyote na wahusika walimuhakikishia kuwa hakutatokea dosari yoyote.

“Kushindwa upigaji nyimbo za taifa ni upungufu mkubwa kiutendaji na kama nilivyosema hapo awali ni aibu kwa taifa letu, napenda kwa niaba ya tff kuomba radhi kwa Mheshiwa Rais, wapenzi waliofurika uwanjani, Watanzania kwa jumla na wageni wetu kutoka Morocco” alisema tenga.

Alisema kuanzia sasa, hata kama mitambo ya uwanjani ni mizima, patakuwepo bendi za police/jeshi ama mitambo ya tahadhari kwa ajili ya nyimbo za taifa na matangazo mengine muhimu.

Source: Michuzi Blog
 
safi sana hiyo!
tenga kweli umetengamaa
 
Source:Michuzi blog
 
..... Wamemuonea rais aliyeingia madarakani kwa rushwa za epa, kagoda lazima vyombo vigome!! Hana kosa. Uonevu tu!!
 
Hizi aibu nyingine ni za kujitakia tu. Hivi huwa hawana 'back up' system?
 
..... Wamemuonea rais aliyeingia madarakani kwa rushwa za epa, kagoda lazima vyombo vigome!! Hana kosa. Uonevu tu!!

hivi hamuwezi kutuacha sisi wenye interest nyingine kujadili mambo zaidi ya upupu wenu?
 
Alitakiwa awajibishwe au awajibike mtu pale pale ilipotokea mara ya kwanza; isingetokea kwa mara ya pili.
 
.......funika kombe mwanaharamu apite..............
 
anacheza huyo na yeye anahusika na upuuzi huo..kwa nini awakumsimamisha wakati wa brasil waliiogopa brasil ama???Kama ungeweza kumwajibisha wakati wa brasil huu upuuzi usingekuwepo we unaona anaogopa rais pekee wakati mpira umeangaliwa DUNIA nzima..ni aibu tupu binafsi ningeanza na TENGA Kwanza awajibike waje hawa kasuku

na mleta mada rekebisha kichwa cha habari amesimamishwa tofauti na amepigwa chini..maana yake arudi tena so far mpaka ajitete kama ulikuwa ujui ndipo wanaangalia nexty adhabu so far bado ni mfanyakazi wa TFF..ila wamechelewa kumtunza hiyo shahada
 
Aina nyingine ya kampeni za Kikwete.... ubabe na kukomoa watu

Mbona timu ilifungwa mbele yake? Kwanini wasimfukuze kocha au kwa nini wasivunje timu?
 
Pamoja na kusemwa kuwa Kaijage kaonewa, hata hivyo siku za karibuni amekuwa na mapungufu mengi katika utendaji wake. Waandishi wa habari watanisaidia kwa hili.
 
we kaijagem jitetee kuwa JK ana gundu ndo maana nyimbo zinagoma mbona akiwa mgeni rasmi mtu mwingine ngoma zinapiga kama fiesta flan hivi
 
umeona eeeh hata alipokuja na brasil ikakataa kuimba y him??
 
Jamani huyo Kaijage si aliwahi kutimuliwa Channel 10 akiwa kituo cha Arusha ?
 
Unaweza kuta vyombo na CD zilijaribiwa na zilikuwa safi, lakini mwendesha mitambo alichefuliwa na ujio wa JK kiwanjani hapo na kugawiwa kwa vipeperushi vya CHAGUA CCM, CHAGUA KIKWETE na ndio maana akaamua kumuhujumu!!
 
Very crap kwa kweli.
yaani TFF mnaandaa cd ya wimbo wa taifa ndo upigwe mbele ya amiri jeshi? Msiige ulaya ambapo wenzenu wanajua maana ya viwango.

Waacheni brass za majeshi ziendelee kutuongoza kuziimba hizi nyimbo na huo uwe utamaduni wetu
pole kaijage
 
Hivi kwa nini wasitumie computer au flash badala ya CD? siyo mtaalamu sana, lakini nafikiri flash hazina tatizo la kukwama kama CD
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…