hata kama tenga angekua competent vipi, michezo kwa wabongo ni last option, na hata wadau wake hawako serious... chunguza kuanzia kamati za soka, vilabu nk.... soka la bongo uswahili mwingi na fitnaIt is high time acha waanze na hicho kishoia na hao wakina tenga natumaini wako njiani. Kinachowaponza ni 10% wanatutia aibu kabisa, tazama wakati wa mechi ya brazil unaona kwenye screen desktop ya computer ya mtu, uwanja wa kisasa tabia za kishenzi. Hiyo mechi ya juzi hata wenye VVIP tickets hawakuweza kukaa kwenye nafasi zao eti zimekaliwa na watu na hapo njiani watu wamejaa vibarabarani, sehemu ya 'non smokers' watu wanavuta mpaka bangi, polisi waliokua wanagombana na watazamaji wamepotea mara tu mechi ilipoanza. Vyoo yavieleweki hao watu waliokaa milangoni ni shida shida shida hawajua lolote wanaendeleza umamluki wa vilabuni. Unataka kuniambia Tenga hajui hayo? kazi kugawana tenda tu na kututia aibu, hebu fikiria yale mangunzo pale uwanjani yule mchezaji wa moroco kaanguka nalo. These people are not serious wanachojua ni kusubiri kualikwa Ikulu kula na raisi. Sasa kwa nini hatua hazikuchukuliwa wakati wa mechi ya brazil? Tenga na kundi lake wanashindwa kuwaelimisha watanzania wanawaacha wanafanya mambo ya ajabu, wimbo wa taifa wa morocco unapigwa watu hawasimami wala kunyamaza, timu wageni wanaignia uwanjani watu wanazomea, jamani tuna laana gani? Toa Leodgar Tenga toa takataka zote hizo recruitment ifanyike properly kwa management ya uwanja wa kimataifa hivi hawaoni viwanja vya wenzetu vinavyohudumiwa? nimekua na very low opinion na Tenga sasa huo ndio usomi? kazi kujipendekeza kwa JK crap kabisa wasimamishwe wote na huyo florian asirudi kabisa tumechoka na migogoro yake na waandishi wa habari za michezo, hatumtaki kabisa.
hata kama tenga angekua competent vipi, michezo kwa wabongo ni last option, na hata wadau wake hawako serious... chunguza kuanzia kamati za soka, vilabu nk.... soka la bongo uswahili mwingi na fitna
Tenga was not even supposed to be there in the first place
Kasheshe, you are right. Kwa aibu hii mbele ya Rais wa nchi, Tenga mwenyewe alitakiwa ajiuzulu. Ingekuwa sawa kumuwajibisha Kaijage kama yeye tenga angekuwa amegundua hiyo itilafu kabla ya kuaibika mbele ya umma.Kwa uzito wa jambo lenyewe Tenga alitakiwa aachie ngazi yeye! Tungemrudisha kwa heshima baadaye!!! lakini kuonyesha alichukizwa yeye ndiye alitakiwa aondoke.
wadau mimi hili suala la kaijage kufukuzwa kwa kushindwa kusimamia suala la nyimbo za taifa (national anthems) siku tanzania na morocco walipocheza naona halijakaa vema. Maswali yangu ninayojiuliza ni haya:-
- kama tff kupitia kaijage walimpa mtu kazi, kwa tenda, ili atumbuize siku hiyo, mwenye dhamana ya kutoa tenda ni "msemaji wa tff" au mtu mwenye dhamana ya procurement? Kwenye tender document si kuna mkataba na unaelekeza nini huyo atakaye tumbuiza afanye siku hiyo na endapo hataweza kuna hatua za kuchukua? (au tff kupitia kwa bw tenga walitoa tenda kienyeji?? Kama sheria ya procurement haikufuatwa basi uwajibikaji ni kwa wengi, si kaijage pekee....
- kwa uozo huu uliofanywa mimi naona tenga na timu yake wote wangejiuzulu kwa dhana ile ya collective responsibility maana ni tff nzima, si kaijage pekee aliyechemsha. Kama tenga anamuona kaijage hakutimiza wajibu yeye kama msimamizi mkuu wa shughuli za tff alichukua hatu agani kuhakukisha kuwa timu yake imejipanga vema na kuwa kila kitu kilikuwa tayari (na alipaswa kufika uwanjani kucheki at least hours before)...sasa kama wote walikuwa busy kufuatilia hela za viingilio inakuwaje kumtoa kafara fk pekee??
- nadhani tenga na yeye yupo vicariously liable
Shirikisho La Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemsimamisha kazi afisa habari wake, Florian Kaijage (pichani) kutokana na fedheha ya kushindwa kutimiza itifaki muhimu ya kupiga nyimbo za taifa wakati wa mechi ya Taifa Stars na Morocco jumamosi jijini.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga amewaambia waandishi wa habari jijini leo kuwa tukio hilo ni la aibu mbele ya Rais Jakaya Kikwete, mashabiki na wageni wengine na mbaya zaidi kwa vile mchezo huo ulionyeshwa katika luninga ndani na nje ya nchi, hivyo aibu hiyo imeshuhudiwa na wapenzi wa soka kote duniani.
Amesema TFF imemua kumwajibisha Kaijage kwa kuwa ndiye aliyekuwa amepewa jukumu la kusimamia jambo hilo. Aidha alisema wakati amesimamishwa kaijage ataisaidia timu itakayoundwa kuchunguza jambo hilo na kuongeza kuwa hatua zitachukuliwa kwa yeyote Yule atakayebainika kuhusika kwa tukio hilo.
Amesema jambo hilo halikustahili kutokea kwa kuwa liliishawahi kutokea wakati wa mchezo na Brazil ambapo safari hii wahusika walipewa jukumu la kuhakikisha kuwa wanazijaribu nyimbo zote siku mbili kabla ya mchezo na kuhakikisha kuwa hakuna hitilafu yoyote na wahusika walimuhakikishia kuwa hakutatokea dosari yoyote.
Kushindwa upigaji nyimbo za taifa ni upungufu mkubwa kiutendaji na kama nilivyosema hapo awali ni aibu kwa taifa letu, napenda kwa niaba ya tff kuomba radhi kwa Mheshiwa Rais, wapenzi waliofurika uwanjani, Watanzania kwa jumla na wageni wetu kutoka Morocco alisema tenga.
Alisema kuanzia sasa, hata kama mitambo ya uwanjani ni mizima, patakuwepo bendi za police/jeshi ama mitambo ya tahadhari kwa ajili ya nyimbo za taifa na matangazo mengine muhimu.
Source: Michuzi Blog
Tenga: you are too trigger-happy to apportion blame but you are a reluctant warrior to assume responsibility. This is a sign of a poor leader and that is what you have always been...
Hivi, Tenga huoni na wewe unapaswa kuwajibika kwa Taifa Stars kufungwa nyumbani hususani kwa kumwalika Bw, Mikosi JK?
Teknolojia imewekwa uwanjani kwa kazi gani ikiwa kila mara lazima tusombe bendi za Polisi, JKT, Jeshi kuja kupiga nyimbo za mataifa kwenye mechi za mpira? Imepitwa na wakati hiyo. Hao watakuja kwenye sherehe za kitaifa au za kijeshi. Kaijage anastahili yaliyomkuta. Mark you, hiyo siyo adhabu. Ni kumfanya apumzike ili uchunguzi ufanyike. We are fed up with mediocrity in every corner and crevice.Kwani lazima tucheze tape(CD), kwani hatuwezi kuimba live nyimbo za taifa? Nakumbuka zamani jeshi la police walikuwa wanatufanyia hiyo kazi na wote mnafurahi. Ukiwauliza TFF watakwambia gharama ni kubwa! Aibu tuliyoipata si ndo kubwa zaidi?
Tenga na kundi lake wanashindwa kuwaelimisha watanzania wanawaacha wanafanya mambo ya ajabu, wimbo wa taifa wa morocco unapigwa watu hawasimami wala kunyamaza, timu wageni wanaignia uwanjani watu wanazomea, jamani tuna laana gani? .
It is high time acha waanze na hicho kishoia na hao wakina tenga natumaini wako njiani. Kinachowaponza ni 10% wanatutia aibu kabisa, tazama wakati wa mechi ya brazil unaona kwenye screen desktop ya computer ya mtu, uwanja wa kisasa tabia za kishenzi. Hiyo mechi ya juzi hata wenye VVIP tickets hawakuweza kukaa kwenye nafasi zao eti zimekaliwa na watu na hapo njiani watu wamejaa vibarabarani, sehemu ya 'non smokers' watu wanavuta mpaka bangi, polisi waliokua wanagombana na watazamaji wamepotea mara tu mechi ilipoanza. Vyoo yavieleweki hao watu waliokaa milangoni ni shida shida shida hawajua lolote wanaendeleza umamluki wa vilabuni. Unataka kuniambia Tenga hajui hayo? kazi kugawana tenda tu na kututia aibu, hebu fikiria yale mangunzo pale uwanjani yule mchezaji wa moroco kaanguka nalo. These people are not serious wanachojua ni kusubiri kualikwa Ikulu kula na raisi. Sasa kwa nini hatua hazikuchukuliwa wakati wa mechi ya brazil? Tenga na kundi lake wanashindwa kuwaelimisha watanzania wanawaacha wanafanya mambo ya ajabu, wimbo wa taifa wa morocco unapigwa watu hawasimami wala kunyamaza, timu wageni wanaignia uwanjani watu wanazomea, jamani tuna laana gani? Toa Leodgar Tenga toa takataka zote hizo recruitment ifanyike properly kwa management ya uwanja wa kimataifa hivi hawaoni viwanja vya wenzetu vinavyohudumiwa? nimekua na very low opinion na Tenga sasa huo ndio usomi? kazi kujipendekeza kwa JK crap kabisa wasimamishwe wote na huyo florian asirudi kabisa tumechoka na migogoro yake na waandishi wa habari za michezo, hatumtaki kabisa.
Upuuzi mtupu. Wanajaribu kutupooza kwa kumsimamisha Kaijage ambaye katolewa kafara wakati wenye makosa ni wao weneyewe. Tenga ndiye anayetakiwa kujiuzulu kama mwenyekiti wa kwani TFF ndio walioharibu sio Kaijage peke yake.