Floyd Mayweather ajitolea kugharamia mazishi ya George Floyd

Floyd Mayweather ajitolea kugharamia mazishi ya George Floyd

Go fund me ya Floyd ina zaidi ya $11Millioni

Go fund me ya mtoto wake wa miaka 6 ina zaidi ya $200,000.

Go fund me ya mdogo wa Floyd ina zaidi ya $300,000.

Go fund me ya ndugu mwingine wa Floyd ina zaidi ya $200,000.

Ukisikia kufa kufaana ndio huku.
 
Bingwa mara tano wa ndondi duniani Floyd Mayweather amejitolea kulipia gharama za mazishi ya George Floyd ambazo zinanakadiriwa kufikia Bilioni 10 za Kitanzania hadi sasa, aliyekufa akiwa mikononi mwa polisi mjini Minneapolis.

Maandamano yamerindima nchini Marekani na hata sehemu nyingine duniani baada ya George Floyd, Mmarekani mweusi kufariki dunia baada ya kugandamizwa shingoni na polisi mzungu wakati akikamatwa.

Polisi huyo Derek Chauvin, 44, ameshtakiwa kwa mauaji.

Taarifa kadhaa kutoka Marekani zinasema familia ya Floyd imekubali msaada wa Mayweather.

Mayweather, 43, ambaye โ€œameguswaโ€ sana na jambo hili atalipia gharama za mazishi mjini Houston, Minnesota na Charlotte.

Familia ya Bw Floyd pia inafikiria kuwa na shughuli nyingine ya mazishi ambayo Mayweather pia amejitolea kuigharamia, kwa mujibu wa Hollywood Unlocked. โ€œNajua atanikasirikia kwa kusema jambo hili, lakini ni kweli, atalitoa gharama za mazishi,โ€ amesema Leonard Ellerbe, Mkurugenzi wa Mayweather Promotions, akizungumza na ESPN. โ€œFloyd amefanya fadhila kama hizi katika miaka 20 iliyopita.โ€ Amesema.

=====

View attachment 1466629

Floyd Mayweather will pay for the funeral services for George Floyd, according to a Mayweather representative.

Floyd, who was black, died last week in Minneapolis after Derek Chauvin, a white police officer, kneeled on his neck for more than eight minutes. Chauvin, who was fired on Tuesday, was charged Friday with third-degree murder and second-degree manslaughter.

Floyd's death sparked protests across the United States over the weekend

"He'll probably get mad at me for saying that, but yes, [Mayweather] is definitely paying for the funeral," Leonard Ellerbe, the CEO of Mayweather Promotions, told ESPN on Monday.

Ellerbe added that the former five-division world champion has been in touch with the family of Floyd, and the family has accepted the offer.

"Floyd has done these kind of things over the last 20 years," said Ellerbe, who added that Mayweather didn't want to talk about his gesture.

Mayweather previously stepped in to cover the funeral expenses of former boxer Genaro Hernandez, who died of cancer at age 45 in 2011. Mayweather won his first world title by defeating Hernandez in 1998.
Mtoa mada inabid uwe unafanya utafit kabla ya kupost.. maiweza ametoa 80000usd around 204 million tz. Sio billion kumi bna..
 
Mtoa mada inabid uwe unafanya utafit kabla ya kupost.. maiweza ametoa 80000usd around 204 million tz. Sio billion kumi bna..
Kijana wangu embu fuatilia tena kww umakini, news za Floyd ziko updated kila baada ya dakika 5, gharama za mazishi zimeongezeka na hio ni kutokana na kua watu wengi sana watahudhuria ikiwemo watu mashuhuri ulimwenguni kama Obama, Biden, Jay Z, na wengineo, hivyo yeye amejitolea kugharamia costs zote ambazo zimeshafikia hicho kiwango
 
Halafu baada ya mazishi,familia yake na watoto wanaendelea kuishi na umasikini,hapa ndio utakapojua ule usemi wa kila mtu na ale kwa jasho lake unapofanya kazi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bilioni kumi wanazika sayari ipi?
Taarifa ya kiinglishi haina costs, ila translation imekuja na 10B...things usually get lost in translation, hii 2020 things gained in translation...

Everyday is Saturday........................... ๐Ÿ˜Ž
 
Na tayari imeshagundulika kuwa alikuwa muathirika wa Covid-19,sasa hiyo hela si robo tatu angempa mke na watoto/mtoto wa marehemu na iliobakia ndio iingie kwenye mazishi,maana msiba hapo hakuna kutokana na nchi kuwa kwenye lockdown...
 
Halafu baada ya mazishi,familia yake na watoto wanaendelea kuishi na umasikini,hapa ndio utakapojua ule usemi wa kila mtu na ale kwa jasho lake unapofanya kazi...

Sent using Jamii Forums mobile app
nani kakudanganya mkuu, wamekwishachangiwa mabilioni hadi sasa, na bado kuna kesi zinaunguruma mahakamani, fidia zake zitakua si mchezo hao wameshakua matajiri.
 
Back
Top Bottom