Floyd Mayweather ashinda pambano la dakika 9 na kuondoka na Tsh. Bilioni 46.9

Floyd Mayweather ashinda pambano la dakika 9 na kuondoka na Tsh. Bilioni 46.9

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Bondia Floyd Mayweather leo amerudi ulingoni dhidi ya Bondia Mjapan Mikuru Asakura katika pambano la maonesho la uzito huru lililochezwa Japan.
1664104032851.png

Katika pambano hilo Mayweather amefanikiwa kushinda kwa KO round ya 2 na kufanya pambo hilo limalizike, Mayweather kabla ya pambano hilo alikuwa amepigana jumla ya mapambo 50 na kushinda yote.

Mayweather alistaafu kucheza professional boxing 2017 na sasa amekuwa akicheza ngumi za maonesho mara kadhaa pale anapokuwa anahitajika.
1664104444737.png
 
Mkuu, jamaa anajua! usimchukulie poa! fikiria mapambano 50 na yote ameshinda, sio mchezo.
Nilibahatika kiliona lile na Manny Pacquiao niseme tu ALIBEBWA. Nataman leo pale ukumbini Pacman angeomba rematch. Inawezekana mengine aliyoshinda kwa points alikua akibebwa kama hilo na Pacman
 
Nilibahatika kiliona lile na Manny Pacquiao niseme tu ALIBEBWA. Nataman leo pale ukumbini Pacman angeomba rematch. Inawezekana mengine aliyoshinda kwa points alikua akibebwa kama hilo na Pacman
Mimi nilikuwa team pac man! Lile pambano ukiangalia kiufundi pacman alipiga ngumi nyingi lakini hazikuwa za point.
Money man kila akishashumbulia alikuwa anarudi na point.
Halikuwa pambano zuri hata hivyo....
 
Nilibahatika kiliona lile na Manny Pacquiao niseme tu ALIBEBWA. Nataman leo pale ukumbini Pacman angeomba rematch. Inawezekana mengine aliyoshinda kwa points alikua akibebwa kama hilo na Pacman
kubebwa kwenye ngumi sio jambo rahisi maana kama angekua mzembe angetandikwa moja akazima,ila kama anabebwa anabebeka huyo ni mkali
 
kubebwa kwenye ngumi sio jambo rahisi maana kama angekua mzembe angetandikwa moja akazima,ila kama anabebwa anabebeka huyo ni mkali
Kubebwa ni rahisi bana kwenye ngumi. Kwani ule usemi kua ukitaka kushinda ngumi utangazwe mshindi nyumbani kwa mpinzani wako basi huna budi kupiga KO ulianzia wapi ? Si ni kwenye hizi hizi mambo za kubebana?
 
Back
Top Bottom