Floyd Mayweather awashindanisha warembo wawili kuhesabu haraka dola laki moja kitandani kwake

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
BONDIA Floyd Mayweather ameonesha jeuri ya pesa ndefu baada ya kuchukua warembo wawili na kuwashindanisha kuhesabu pesa zinazofikia dola laki moja akiwa kitandani kwake, huku akitumia saa yake kuangalia nani anahesabu haraka zaidi.

Mayweather alishinda mchezo jumamosi iliyopita dhidi ya Marcos Maidana mjini Las Vegas na kuchukua ubingwa uzito wa welterweight na kuendeleza rekodi ya kutopoteza katika michezo 46 ya kimataifa na ameshangilia ubingwa wake kwa kuwashindanisha warembo kuhesabu `mkwanja` wake.


Wakizitawanya: Mayweather akihesabu dakika, huku warembo wakishindana kuhesabu haraka dola
laki moja kitandani kwa bondia huyo.



Mmarekani huyo akiwa na kibegi kidogo chenye saa 18 aliandika maneno yafuatayo: ” THAtjessilee na badmedina wanacheza mchezo, kuona nani anaweza kuhesabu dola laki moja ( $100,0000) kwa haraka zaidi. Hivi ndivyo wanafanya wakichoka. #TheMoneyTeam #FollowBeautifulLadies ’.

Ni haki yake kusema dola laki moja ni fedha kidogo kwa bondia huyo bingwa mara tano wa dunia, ambaye alipata dola milioni 70 kutokana na pambano lake dhidi ya Maidana.


Mayweather akionesha vito vya thamani

Alipata dola milioni 32 kenye mchezo uliopigwa MGM Grand , na vilevile anasema anapata dola milioni 38 kutokana na matangazo ya televisheni.
Wanawake wawili, Jessi Lee na Doralie Medina walipigwa picha wakiwa kama sehemu ya wasaidizi wa timu ya Mayweather, inayojulikana kama Timu ya hela ` The Money Team (TMT)`.
 

Attachments

  • tmt 2.jpg
    45.3 KB · Views: 3,074
  • tmt.jpg
    38.5 KB · Views: 3,073
Last edited by a moderator:
Ngoja kwanza, bado kidogo tutasikia anakesi ya kubaka mara kakutwa na silaha bila kibali ,mara kampiga mtu disko, mara kaendesha gari kwa kasi akiwa amelewa ilimradi wamfirisi tu.!
 
Ngoja kwanza, bado kidogo tutasikia anakesi ya kubaka mara kakutwa na silaha bila kibali ,mara kampiga mtu disko, mara kaendesha gari kwa kasi akiwa amelewa ilimradi wamfirisi tu.!

Media Attention
 
apigane na pac man ndiyo ntakubali yuko fit
 
Ngoja kwanza, bado kidogo tutasikia anakesi ya kubaka mara kakutwa na silaha bila kibali ,mara kampiga mtu disko, mara kaendesha gari kwa kasi akiwa amelewa ilimradi wamfirisi tu.!

halafu soon anajiunga na timu ya waliofilisika akichukua no.3 baada ya evander na tyson
 
Watu weusi, esp wanamichezo, wanamuziki/rappers.......siku zote wanaishia kuwa RICH badala ya kuwa WEALTHY.........na moja ya sababu kubwa ni ULIMBUKENI a.k.a masikini akipata kalio linalia mbwata.....na zikiisha wanasema wazungu ndio wanawabania.....
 

Kuna watu wanajiita platinum! Hapa Tz ngoja waje!
 
Last edited by a moderator:
huyo afadhali kuna yule pimbi mwenzake ambaye anamgeza wa kuitwa adrien broner!...........hamnaga tajiri wa kiarabu mwenye upimbi huu
Huyu ndo pambavu anamwiga floyd kila kitu,tabia,kiburi,juzi baada ya kushinda alitoa maneno ya kibaguzi kwa boxer wa mexico na WBC wamemfungia mpaka aombe radhi...
 
wapi kaka cheka, miyeyusho bila kumsahau mashali....????? :boxing:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…