kaka Kilbark, you are right, mimi nafurahi sana kuona Vijana wenye mawazo ya Kimapinduzi, it is fantastic, hasa kuhusu suala la kujiendesha yenyewe na kuacha Raisi kuteua mtu kuiongoza hiyo ATCL, ni jambo la maana sana, yaani Raisi wa nchi anafanya kazi zingine hata zisizokuwa na tija, kuhusu suala hili Watanzania tunatakiwa kuchukua haatua kuiendesha ATCL kwa kuuziwa hisa kama wanavofanya Kenya airways, we angalia shirika la kenya lilivokuwa superb, kwanini? ni kutokana na kuwa serikali imejiondoa toka zamani na kuwaachia waKenya waliendeshe, kwanini serikali inag'ang'ania kuliendesha, kuna kitu gani hapo au ndo hiyo mikataba ambayo kila siku inachangia kuliua shirika letu,hii haitiii akilini kabisa. Mimi nimeshaapa kuwa sitapanda tena Precision na ndo maana nataka kubadilisha route zangu zote za safari, nataka ndege inayoenda straight to Dar from abroad baadala ya Kupitia Kenya ambako unakutana na Precision, vindege vyenyewe kelele tu mpaka mtu kichwa kinataka kuchomoka, yaani unatamani ufike haraka Dar badala ya kuinjoy safari---Hell no! lazima tuamke jamani. na serikali Jitoeni basi sisi tuwekeze.
Rom